Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Akida Khea akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mapema wakati wa kutangaza matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa vifaa tiba, vitendanishi, dawa asili na tiba mbadala, tukio lililofanyika makao makuu ya TMDA, Mabibo Jijini Dar e Salaam.
Na Asha Mwakyonde
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imebaini aina saba za
dawa bandia katika ukaguzi maaluma wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na
dawa asili za tiba mbadala ambazo zinathamani ya Sh. Milioni 12. 5.
Ukaguzi huo maalumu ulifanyika kwa kushirikiana na ofisi ya
Rais, Baraza la Famasia, Baraza la Dawa Asili na Tiba Mbadala na ofisi
ya Rais (Tamisemi) Oktoba 8 hadi 11 mwaka huu katika maeneo 558
kwenye wilaya 33 za Mikoa 20.
Akizungumza na waandishi wa habari keo Novemba 13 , 2019
jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Akida Khea alisema
dawa zilizokamatwa ni Sonader Cream 10gm, Gentrisone Cream 10gm,
Sulphadoxine Pyrimethamine, Alprim, Homidium Chloride, Cold cap na
Temeva NDV strain.
“Hizi dawa tumebaini ni bandia baada ya operation maalum
iliyofanyika kuna Sodium cream toleo namba A1912 na A1758 ni bandia,
Gentrison cream toleo namba GNTRO X031 na tarehe ya kutengenezwa
21/04/2019 ni bandia.
“Kuna za kopo =ambazo ni Sulphadoxine Primethamine hii
kopo la dawa husika lina namba ya kughushi ya usajili namba TAN
05.412.102.FAST kuna Alprim toleo namba 6L74 na tarehe ya kutengenezwa
ya Oktoba 2018 ni bandia.
“Homidium Chloride makopo matatu ya dawa hii ya mifugo
inaonekana kutengenzwa na ki9wanda cha Ciplaya India ambacho
hakitengenezi dawa za mifugo na makopo mengine suta yanaonesha
yametengenezwa na kiwanda cha Malleus Chem Ltd ya Kenya taarifa ambazo
sio ya kweli na ni bandia.
“Zingine ni Cold cap dawa hii inadaiwa kutengenezwa nchini
India ambapo jina la kiwanda haipo kwenye kifungashio wakati dawa halisi
ni COLDCAP ambayo inatengenezwa na kiwanda cha REGAL Pharmaceuticals
Ltd cha Kenya.
“Dawa nyingine ni Temevac NDV strain 1 na 2 dawa hii bandia
umeandikwa kwa kiingereza na inamakosa ya kisarufi katika lebo dawa
hizi hasi zinatengenezwa na kiwanda cha serikali cha TVI na
imethibitisha kuwa dawa hizi ni bandi,”alisema Khea.
Kwa mujibu wa Khea katika ukaguzi uliofanyika pia dawa
ambazo hazijasajiliwa zilikamatwa zenye thamani ya Sh 31,934,360 na dawa
za Serikali zenye thamani ya Sh 481,600.
“Dawa hizo ambazo hazijasajiliwa zilikuwa ni kapsuli za
dawa inayotambulika kwa jina la Indowin, vidonge vya dawa vyenye
mchanganyiko wa Artesunate na Amodiaquine,kapsuli za dawa iliyojulikana
kwa jina la Coldwin na dawa ya sindano ya Magnesium Sulphate.
“Dawa za Serikali zilizokamatwa ni chupa za dawa na sindano
ya oxytocin, vidoge aina ya Bigomet, vichupa tisa, dawa za vidongo
yenye kutibu malaria na zingine pia zilikamatwa katika maduka ya watu
binafsi.
“Pia tulikamata vifaa tiba vyenye thamani ya Sh 640,000
kati yake ikiwa ni Sugical blades na H.pylori rapid test na vifaa tiba
vya serikali vyenye thamani ya Sh 224,300, operation pia ilibaini vifaa
tiba ambavyo havujasajiliwa vyenye thamani ya Sh 16,384,750,”alibainisha
Khea.
Alisema kutokana ukaguzi huo mpaka sasa watuhumiwa
wameshafikishwa katika vyombo vya usalama ambapo jumla ya majalada 19 ya
kesi yameshafunguliwa katika vituo mbalimbali vya polisi.
“Aidha ufuatiliaji kupitia vyombo vya usalama unaendelea
kuwabaini wale wote waliojihusisha na uingizaji ,utengenezaji na
usambazaji wa dawa bandia.
Khea alisisitiza kuwa pamoja akubainika kwa uwepo wa dawa
na vifaa bandia lakini zipo dawa halisi na zilizosajiliwa na TMDA zenye
majina kama hayo.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuhakiksha wanapata
dawa kutoka katika vituo vya kutolea huduma za dawa vunavyotambuliwa na
serikali ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa yaliyosajiliwa na serikali
kupitia taasisi zake na kupewa risiti baada ya kununua.
“Endapo watabaini kuwa matoleo ya dawa zilizobainishwa kuwa
ni bandi wanashauriwa kuzirudisha dawa hizo katika ofisi za TMDA au
ofisi za serikali zilizo karibu na wao na kwa lengo la kulinda afya ya
jamii wananchi wanaombwa kutoa taarifa kuhusu mtandao wa wale wote
wanaojihusisha na usambazaji,utengenezaji, uingizaji na wiziwa
dawa,vitendanishi na vifaa tiba vya bandia au vya serikali.
No comments:
Post a Comment