Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza
Dk. Gwajima alifanya ziara ya kukagua ujenzi huo Novemba 7, 2019 na kisha kuelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuanza taratibu za kuhakikisha hospitali hiyo inaanza kutoa huduma kuanzia mapema mwaka ujao, ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi.
Naye Msanifu Majengo Mwandamizi OR- TAMISEMI, Jonaphry Rwabagabo, alitoa rai kwa wahandisi katika Halmashauri nyingine 67 nchini, zinazojenga Hospitali za Wilaya kutimiza vyema majukumu yao ili kuhakikisha wanatekeleza kwa ubora miradi hiyo kama ilivyoonekana katika majengo ya Hospitali ya Wilaya Ilemela.
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela ulianza Machi mwaka huu kwa kutumia mfumo wa 'Force Account' ambapo Serikali ilitoa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Majengo mbalimbali ya Hospitali ya Wilaya Ilemela yanayojengwa katika Kata ya Sangabuye (eneo la Kabusungu-Isanzu).
Mwonekano wa majengo mbalimbali.
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela uko katika hatua za mwisho ambazo ni pamoja na kuweka milango pamoja na madirisha.
Ukaguzi ukiendelea katika Hospitali ya Wilaya Ilemela.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI), Dk. Dorothy Gwajima, akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa huduma za afya mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment