HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 30, 2019

WATAKAOAJIRI WATOTO CHINI YA MIAKA 18 KWENYE TUMBAKU KUKIONA CHA MOTO – MHE HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 30 Novemba 2019 kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dar es Salaam.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesisitiza marufuku yake aliyoitoa hivi karibuni kuhusu ajira kwa watoto ambao wapo chini ya miaka 18.

Mhe Hasunga amepiga marufuku hiyo leo tarehe 30 Novemba 2019 wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa suala la ajira kwa watoto ni miongoni mwa mambo yanazuiliwa kwenye Sheria za kimataifa kupitia Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization) na Sheria za Ajira hapa nchini hivyo mdau yeyote atakayebainika kukiukwa maelekezo hayo atashtakiwa.

“Nawasihi wadau wote hususani wakulima wa Tumbaku tuendelee kupiga vita ajira kwa watoto kwa kuwa ni eneo ambalo limeendelea kulalamikiwa na wadau wengi” Alikaririwa Mhe Hasunga

Kadhalika, Mhe Hasunga alisema kuwa katika kuhakikisha zao la tumbaku linaendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la mkulima na Taifa, Wizara imejiwekea malengo ya haraka yanayopaswa kutekelezwa ambayo ni pamoja na usajili wa wakulima wote wa tumbaku, kuwapatia vitambulisho na kuwaingiza kwenye kanzidata ili kupata takwimu za uhakika za maeneo wanayolima na kuiwezesha serikali kusimamia upatikanaji wa pembejeo kulingana na mahitaji yao.

No comments:

Post a Comment

Pages