Meneja Masoko wa Vodacom M-pesa, Noel Mazoya, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupata punguzo wanapofanya malipo kupitia huduma ya M-Pesa na hasa kwenye kipindi hiki cha ‘Black Friday’, siku maarufu duniani kwa manunuzi ya bidhaa kwenye maduka na mtandaoni. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wafanyabiashara mbalimbali nchini imezindua kampeni kabambe inayowawezesha wateja wake kufurahia punguzo kubwa wanapofanya malipo kupitia huduma yake ya M-Pesa.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es salaam inalenga kuongeza matumizi ya huduma za kidigitali kwenye kufanya malipo hasa kwenye kipindi hiki cha Black Friday, siku maarufu duniani kwa manunuzi ya bidhaa kwenye maduka na mtandaoni.
Kupitia huduma zake mbili za Lipa kwa simu na Mpesa na M-PESA Mastercard Vodacom M-Pesa wanawawezesha watanzania kufanya malipo kwa wafanyabiashara ndani ya nchi na mitandaoni kupitia simu zao na kurudishiwa hadi aslimia 10 ya gharama za malipo siku hiyo ya Black Friday ambayo kwa mwaka 2019 itakuwa Novemba 29.
Meneja masoko wa Vodacom M-Pesa, Noel Mazoya alisema, ‘Black Friday hii tumeandaa ofa ya hadi asilimia 10 ya gharama ambayo wateja wetu watalipa kupitia huduma za Lipa kwa simu na M-PESA MASTERCARD. Kupitia huduma ya Lipa kwa simu, M-Pesa tutawarudishia hadi asilimia 10 papo hapo wakilipa kupitia mtandao wowote kwenye maduka mbalimbali yaliyopo kwenye malls tofauti nchini.
Baadhi ya maduka kwa Dar es Salaam ni Mlimani City (Mr Price, Just Fit sports gear, Atsoko, Cassandra Julac, Joo Africa na Vodashop Mlimani, Dar Free Market (Home of events, Zurii house of beauty, Vodacom service desk) City Mall (Kanzu Point, Ley Jewerly, G Best Zone), Rock City Mall Mwanza (Street Soul, Chief Empire Classic, Café Mambo, Upendo Unique beauty shop na Vodashop Rock City) na Aim Mall Arusha (Street Soul, Supa Clean) na mengineyo.
Meneja uendeshaji wa Mr. Price Tanzania, Paul Namuhisa alisema ‘Tunafurahi kushirikiana na Vodacom katika kampeni hii. Pamoja na punguzo la hadi asilima 10 ukinunua bidhaa kupitia M-Pesa, Tunatoa punguzo la asilimia 20 kwa manunuzi ya bidhaa kwa siku hiyo, huu ni muendelezo wa utamaduni wetu wa kuleta kitu kipya kwa wateja wetu kila siku’
Kwa Upande mwingine, Vodacom kwa ushikiriano na Easybuy Africa itawarudishia wateja hadi asilimia 10 ya kiasi watakacholipa kwa M-PESA Mastercard kupitia tovuti ya www.easybuyAfrica.com.
Wateja watarudishiwa hadi asilimia 10 wakifanya shopping kutoka mitandao kama Amazon.com, eBay, H&M, Walmart, GAP, Fashionova kupitia EasyBuyAfrica.com na kulipa kwa M-PESA Mastercard. Pia watafurahia punguzo la hadi asilimia 10 ya oda zao kutoka EasyBuy pamoja na discount za hadi asilimia 85 kutoka tovuti husika siku ya BlackFriday.
Meneja wa Easybuy Afrika, Juliana Siyame alisema, ‘Easybuyafrica inawezesha wateja kununua bidhaa yoyote wanayohitaji kutoka mitandao tofauti duniani na kuwaletea popote walipo Tanzania. Kipindi hiki cha Black Friday tunawawezesha kufurahia huduma zetu kukiwa na punguzo kubwa kwenye bidhaa tofauti pamoja na ofa maalum ya 10% discount wakiagiza nasi Ijumaa. Ushikiriano wetu na M-Pesa Mastercard umeaongeza faida zaidi kwa wateja wetu kwa kuwapa njia salama ya kulipa mtandaoni’

No comments:
Post a Comment