HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 27, 2019

Yoso wa Atletico Madrid atwaa Tuzo ya Golden Boy

Joao Felix

MADRID, HISPANIA

FOWADI yoso wa klabu ya Atletico Madrid ya hapa, Joao Felix, ametangazwa mshindi wa Tuzo ya Golden Boy kama Mchezaji Bora Chpukizi chini ya miaka 21 barani Ulaya, tuzo inayotolewa na Gazeti la Tuttosport la Italia.

Kinda hilo la kimataifa la Ureno, lenye umri wa miaka 20, alifunga mabao 18 akiwa anaichezea Benfica ya nyumbani kwao, kabla ya kuuzwa kwa dau la euro milioni 126 (sawa na pauni milioni 113) kwenda Atletico kiangazi kilichopita.

Tangu kuwasili Hispania, Joao amefunga mabao mawili katika mechi 10 za Ligi Kuu ‘La Liga.’ Yoso wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya vijana ya Uingereza, Jadon Sancho, 19, alshka nafasi ya pili katika tuzo hiyo, huku kiungo wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, akishika ya tatu.

BBC Sport

No comments:

Post a Comment

Pages