Na Lydia Lugakila, Kagera
Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Rushwa Kata ya Mshabago wilayani Muleba mkoani Kagera amekutwa amejinyonga kwa kamba ya katani
na kupoteza maisha.
Mtendaji wa kata hiyo, Goreth
Gervaz, amemtaja aliyejinyonga kuwa ni
Frank Angero mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa kitongoji cha Buyango ambapo taarifa za tukio hilo zimebainika
Decemba 3 mwaka huu kijijini hapo.
Gervaz amesema kuwa marehemu
amekutwa amejinyonga nyumbani kwake kwa kutumia kamba na hakuacha kujumbe
wowote unaoelezea chanzo cha yeye kufanya hivyo.
‘’Kwenye nyumba yake mwenyewe majirani
walisema walifika wakapiga hodi bila kumuona mhusika baada ya kusogeza pazia
wakaona amening’inia na kuwa chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa alisema
mtendaji huyo.
Ameongeza kuwa kwa kipindi cha miezi
mitatu iliyopita marehemu na mke wako walikuwa na migogoro ya kifamilia
iliyosababisha wanamfuata mtendaji huyo hadi maeneo yake ya kazi.
Kwa upande wake shemeji wa marehemu
Edwin kazimili amesema kuwa baada ya kupata taarifa alienda nyumbani kwa
marehemu na kukuta amejinyonga.
Naye mke wa marehemu Jastina Frank
amesemakuwa tukio hilo lilitokea wakati akiwa hayupo nyumbani kwani alikuwa amekwenda kwa
wazazi wake kwa ajili ya kumuona mtoto aliyekuwa anaumwa.
No comments:
Post a Comment