Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika
Yasiyo Ya kiserikali Dkt. Richard Faustine Sambaiga akitoa maagizo kwa Baraza la
Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali akiwataka kufanya marekebisho muhimu ya
uendeshaji wa Chombo hicho na kutoa taarifa ya uzingatiaji wa maagizo kuhuisha
utendaji wao ndani ya kipindi cha siku 30 wakati alipokutana na wajumbe wa
Baraza hilo na baadhi ya waandishi wa habari kwenye kikao kilichofanyika ukumbi
wa NIMR jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali, Nicolaus Zachariah.
Na Mwandishi Wetu Dar
es Salaam
Bodi ya Uratibu wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeliagiza Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali kukutana ili kuhakikisha wanatatua
changamoto za uendeshaji wa Baraza hilo kikamilifu na kutoa taarifa kwa Bodi
ndani ya siku 14 jinsi walivyoshughulikia changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na
kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Baraza hilo.
Agizo hilo limetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dk. Richard Faustine
Sambaiga wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali katika kikao kilicholenga kutoa maelekezo mahsusi kwa Baraza ili
kukitaka chombo hicho kuzingatia matakwa ya kisheria katika uendeshaji wake.
Dk. Sambaiga ameliagiza Baraza hilo kufanya mapitio ya Kanuni
ya Sheria ya marekebisho Na. 11/2005 na Sheria ya marekebisho Na.3/201
ili kuweza kukidhi mapendekezo ya mapitio ya Kanuni hizo na kuwasilisha kwenye
Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ndani ya siku 30 ili kuondoa mkwamo wa
kiutendaji wa majukumu ya Baraza la NGOs nchini.
Pia
Dk. Sambaiga ameliagiza Baraza hilo kujielekeza kwenye
matakwa ya muda wa kisheria wa kuwa kiongozi wa Baraza hilo ambao ni miaka
mitatu toka kuteuliwa kwa Baraza mwaka 2016, na hivyo kuelekeza kuanza kwa
mchakato wa uchaguzi wa Baraza jipya ndani ya siku 30.
“Nalielekeza Baraza kupitia upya
uwakilishi wa wajumbe wa Mikoa na makundi maalum hasa ikizingatiwa ipo Mikoa
mipya na makundi ambayo hayana wawakilishi kwani kumekuwa na changamoto kubwa
ya uwakilishi wa wajumbe kutoka mikoani” alisema.
Aidha Dk. Sambaiga amewataka
Viongozi wa Baraza la Taifa kuzingatia uwasilishaji wa taarifa yake ya
utekelezaji wa kazi zake kwa Bodi ili
kutosababisha Bodi kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kisheria kama
yalivyoainishwa kwenye kifungu 7(1) (j) cha Sheria ya Mashirika yasiyo ya
Kiserikali kinachoitaka Bodi kupokea kujadili na kupitisha taarifa za Baraza
hilo.
Dk. Sambaiga amelitaka Baraza
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ikiwemo kutetea maslahi ya Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali kwa kuwa jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuhakikisha
wanakuwa mwavuli wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika masuala yote
yanayohusu uratibu na kutandaa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali; na
“Nawasihi viongozi wa
Baraza Kutunga
na kusimamia utekelezaji wa Kanuni za Maadili kwa lengo la kuwezesha Mashirika
Yasiyo ya kiserikali kujiongoza kwa
kufuata misingi ya kimaadili yenye uwazi na uwajibikaji.”
Mweyekiti wa Bodi ya Mashirika Yasika
ya Kiserikali ameleza kuwa maelekezo
anayoyatoa yanalenga kuhakikisha kuwa Baraza la Mashirika ya NGOs linatekeleza
kazi zake kikamilifu, kuimarisha uratibu wa sekta ya NGOs, kuondoa chanagmoto
za uendeshaji wa NGOs hivyo Bodi ikalazimika kutoa maagizo thabiti kuboresha
uendeshaji wa kazi za NGOs nchini.
Dk. Simbaiga amelieleza Baraza la Taifa
la NGOs kuwa ulegevu wa kiutendaji ndani ya Baraza la NGOs unakwamisha utendaji
wa kazi za Bodi ya NGOs amabzao wamekasimiwa kuzitekeleza kwa mujibu wa sharia,
kanuni na taratibu.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali, Nicolaus Zachariah ameshukuru kwa hatua iliyochukuliwa
na Mwenyekiti wa Bodi ya NGOs ya kukutana na wajumbe wa Baraza la NGOs na kujadili
masuala yenye chanagamoto katika uendesjai wa majukumu ya Baraza. Baraza la
NGOs limepokea maelekezo ya Bodi na kukiri kuyafanyia kazi maagizo yote kwa
pamoja kama yalivyowasilishwa na Bodi ya NGOs.
Aidha, Baraza la NGOs limeaomba
kuendelea kupata ushauri wa kitaalam na msaada wa kisheria ili kuhakikisha kuwa
maalekezo yote yanatekelezwa katika muda uliokubainishwa.
Bodi ya Uratibu wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali iliyoanzishwa chini ya Kifungu cha 6 (1) cha Sheria ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya Mwaka 2002 kwa lengo la kuwakilisha
Sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ikiwa na jukumu la kusimamia uratibu wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini ikiwemo uendeshaji wa Baraza la Taifa la
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
No comments:
Post a Comment