Na Bryceson Mathias
KAIMU Mwenyekiti wa Mamlaka
ya kuthibiti mbolea nchini, Charles Chenza (pichani), akihojiwa na ITV kwenye
Kipindi cha Dakika 45, amewatuhumu Maafisa Ugani nchini walioko vijijini, akidai
wamekuwa wafanyabiashara ya bodaboda badala ya kutekeleza wajibu wao ili wakulima
wawe na kilimo chenye tija.
Hatua hiyo imewaudhi wengi wa
maafisa ugani waliosikia mahojiano yake
na Mtangazaji wa Kipindi cha Dakika 45, Benjamini Mzinga, ambapo wamesema wao
wanafanya kazi waliyoaminiwa tofauti na tafsiri potofu ya Chenza na kumtaka
awaomba radhi kabla hawajachukua hatua nyingine Kitaifa.
Maafisa ugani hao waliohojiwa
kwa nyakati tofauti kuhusu tuhuma hiyo na walirusha Kilio chao kwa Waziri mwenye
dhamana ya Kilimo ambapo wamedai, Kiongozi huyo amewadhalirisha bila kuwa na chembe
ya Ushahidi kwamba wamekuwa hawapo kwenye sehemu zao za Kazi ya kuwa waendesha biashara
ya bodaboda.
Aidha wameilalamikia Serikali
Kuu wakidai Kauli ya Chenza imewaondolea Ueredi na kuaminika kwao kwa Wananchi
na Serikali, na hivyo hawawezi kutafuta ugomvi na kukosana na Waziri mwenye
dhamana ya Kilimo au Bodi yote ya Mamlaka ya Kudhibiti Mbolea isipokuwa wanaona
mbaya wao ni Chenza.
Akizungumzia uagizaji wa Mbolea, Matumizi na Mwongozo mpya wa manunuzi makubwa ya Mbolea
(Bulk Procurement), Chenza akijimwambafai dhidi ya ufaniisi na matumizi mazuri
ya Mbolea alijikuta akiwachokoza pasi na ugomvi maafisa ugani hao kuwa wamekuwa
bodaboda.
Mmoja wa maafisa ugani
alisema, wanaiomba Serikali Kuu kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya Kilimo kupitia
mahojiano hayo kwenye kipindi hicho ili Chenza ajitathimini na kuthibitisha iwapo
alikuwa na nguvu gani ya kutoa tuhuma hizo nzito dhidi yao kwa kuwajumuisha
wote kama labda aliwahi kumuona moja wao na kumshitakia kwa viongozi wake.
No comments:
Post a Comment