Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo
kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani na wenzake kutoka
Jamhuri ya watu wa China wakimpima mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo
unavyofanya kazi (Echo Cardiogram) kabla ya kumfanyia upasuaji mdogo wa kuziba
tundu la moyo kupitia mshipa wa damu wa
kwenye paja kwa kutumia mashine ya (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography
– TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia
mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo
kwa watoto kutoka Jamhuri ya watu wa China Prof. PAN Xiang Bin akimfanyia mtoto
mwenye umri wa miaka minne ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) upasuaji mdogo wa kuziba tundu la moyo bila kufungua kifua
kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa kutumia mashine ya kipimo cha
kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO machine) bila ya kutumia mionzi
(Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara nyingi upasuaji huo hufanyika kwa
njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory).
Picha 3: Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Jamhuri ya Watu wa China wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kumfanyia mtoto upasuaji mdogo wa kuziba
tundu la moyo bila kufungua kifua kupitia mshipa wa damu wa kwenye paja kwa
kutumia mashine ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO
machine) bila ya kutumia mionzi (Transthoracic Echocardiography – TTE). Mara
nyingi upasuaji huo hufanyika kwa njia ya mionzi kwa kutumia mtambo wa Cathlab
(Catheterization Laboratory). (Picha na JKCI).
No comments:
Post a Comment