Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiangalia handaki lililotumiwa na Samora Mashel lililopo wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiwa ndani ya handaki lililotumiwa na Samora Mashel lililopo wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika.
wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa Afrika.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akimsikiliza Mama Loisa Kamwaya (aliyevaa kilemba) akiwa miongoni mwa Watanzania walioolewa na Wanamimbia waliokaa Wilaya ya Kongwa mkoa wa Dodoma wakati wa kupingania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akiangalia moja ya masalia ya mabomu yaliyotumiwa wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika
eneo la Kongwa mkoani Dodoma.
eneo la Kongwa mkoani Dodoma.
Na Eleuteri Mangi, Kongwa
Serikali inaendelea kubainisha
maeneo yaliyotumiwa na wapingania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika ambayo
yanasimamiwa kupitia Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika iliyopo chini ya Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Akiwa katika ziara ya kikazi
wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakati akitembelea maeneo ya historia ya Ukombozi wa
Afrika, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa Serikali
kupitia wizara hiyo inaandaa sheria ya kulinda na
kuhifadhi urithi wa ukombozi wa
Afrika unaopatikana nchini. “Lengo kubwa ni kuhakikisha
maeneo haya yanalindwa kisheria ili yaweze kutumika kama vivutio vya utalii wa
kiutamaduni pamoja na utalii wa kihistoria kwa sababu huu ni urithi muhimu wa historia
nzuri ya nchi yetu, haya ni maeneo yaliyotumika kusaidia ukombozi wa Nchi za Kusini mwa
Afrika” alisema Naibu Waziri Shonza.
Katika kutekeleza Programu ya
Uhifadhi na Uendelezaji wa historia ya Ukombozi wa Afrika, Wizara inaendelea
kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo, ukarabati wa
jengo lililokuwa la Kamati ya
Ukombozi ya iliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambayo kwa sasa ni Umoja wa
Afrika (AU).
Kazi nyingine ambazo Serikali
imekamilisha ni uandaaji wa tovuti ya Programu, ubainishaji wa maeneo
yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi, utambuzi wa nyaraka na vitu mbalimbali
vinavyohusiana na harakati hizo pamoja na kufanya mahojiano na watu walioshiriki au
kushuhudia harakati za ukombozi wa Afrika ambayo yamehifadhiwa kwa njia ya
kidigitali.
Mji wa Kongwa kihistoria ni
kitovu cha harakati za Ukombozi wa Afrika kwani harakati zote za mapambano ya kutafuta uhuru
zilianzia Kongwa na baadaye zikaendelea katika maeneo mengine nchini kama
sehemu ya kupanua wigo wa harakati hizo na huduma kwa Wapigania Uhuru.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya
hiyo Deogratius Ndejembi amesema kuwa Kongwa ni eneo kongwe lililotumiwa na Wapigania
uhuru kutoka vyama mbalimbali vya Ukombozi kutoka nchi za Kusini
mwa Afrika.
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya
alisema kuwa eneo hilo lilitumika kwa ajili ya mafunzo kwa wapigania uhuru ambapo kwa
sasa lina vielelezo muhimu vya kihistoria vilivyopo katika eneo hilo yakiwemo maeneo
ya Handaki alilokuwa akilitumia Samora Mashel, nyumba za Makazi kwa wapigania
uhuru, majengo ya shule ya sekondari Kongwa, eneo la Mafunzo ya kijeshi, kiwanja
cha ndege na makaburi ya wapigania uhuru.
Maeneo mengine ya kihistoria ni
makaburi ya mashujaa wa harakati za ukombozi ambayo jumla yake ni 11; makaburi
matano ya wapigania uhuru kutoka Msumbiji, makaburi matatu ya wapigania
uhuru kutoka Afrika Kusini na makaburi matatu ya wapigania uhuru kutoka Namibia.
Naibu Waziri Shonza yupo katika
ziara ya kikazi kutembelea maeneo ya ya historia ya ukombozi wa Afrika katika mikoa
ya Dodoma wilaya ya Kongwa, Morogoro wilaya Kilosa, Manispaa ya Morogoro
pamoja na Mkoa wa Pwani wilaya za Chalinze na Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment