Mshindi
wa Mikwaju ya jumla wa mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019 M
Chadha kutoka klabu ya Kili mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa
Mwakilishi kutoka kampuni ya Oryx Energy Sira Muhele katika mashindano
yaliyomlizika katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha.
Mshindi
wa jumla wa mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019 Victor Joseph
kutoka klabu ya Gymkhana mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje Mh Dumbaro katika mashindano yaliyomlizika
katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha.
SELEMANI SEMUNYU
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mh Damas Ndumbaro
amehitimisha Mashindano ya Gofu ya Wazi
ya Tanzania Open jijini Arusha huku mcheza gofu Victor Joseph kutoka klabu ya Gymkhana ya Dar es Salaam
akitwaa ubingwa wa mashindano hayo
Mchezaji huyo kutoka Klabu ya Dar es Salaam
Gymkhana alifanikiwa kubakiza kombe baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo
yaliyoshirikisha wachezaji toka Nchi Sita kwa kupata Mikwaju (Gross) 294.
Siku ya kwanza Mchezaji huyo alicheza 75,74,71 na 74
akifuatiwa Joseph Chinywai kutoka Uganda aliyepata mikwaju 308 na kuwashinda
wachezaji wengine wa divisheni A
walioshiriki mashindano hayo.
Katika Mikwaju ya jumla Net Manraj Chadha wa kili golf
aliibuka na Ushindi baada ya kupata
Mikwaju ya Jumla 291 huku akiwa amecheza 72,74,71 na 74 katika mzunguko
wa Mwisho.
Mshindi katika Divisheni B
ni Joe Lee ambaye alipata mikwaju ya
jumla 149 baada ya kucheza 71 na 78 katika
mzunguko wa pili huku kiwango chake cha makosa kikiwa ni 18.
Mshindi katika kundi la senior ni Boniface Nyiti wa Lugalo
aliyepiga Mikwaju yaa Jumla 162 baada yaa mzunguko wa kwanza kupata mikwaju 81
sawa na mzunguko wa pili huku kiwango cha makosa kikiwa ni Nane.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TGU Criss Martin alisema mashindano haya ni
mashindano ya 69 tangu kuanzishwa kwake lakini kumekuwa na Changamoto nyingi na
kuomba Rais Magufuli kutupia Jicho mchezo huo.
“ tunatambua kazi kubwa ya Mh
Rais katika Majukumu mbalimbali ambayo amekuwa akifanya lakini tunaomba atupie
jicho pia Mchezo huu umekuwa na
mafanikio” Alisema Mwenyekiti.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ndumbaro
aliahidi kufikisha kilio chao kwa wahusika ili kuendeleza mchezo huu nap engine
kwa kuanzia ngazi yaa Mashuleni ili kupata vipaji na kuzalisha wachezaji bora
wakiwemo wa kulipwa
“ Nitafikisha Kilio chenu
Serikali ili kuboresha Mchezo huu lakini pia hakikisheni mnasajili viwanja ili
viwango vya Uchezaji viweze kutambulika Kimataifa “. Alisema Naibu Waziri
Ndumbalo.
Aidha alisema Mashindano
yamefanikiwa na hiyo ni kutokana na Kazi
nzuri waliyofanya kwa kushirikiana na na kamati ,waratibu Verge Africa na
wadhamini ambaao wamefanya Zawadi kuwa Bora hivyo inahitaji kuendelezwa.
Klabu za Tanzania zilzoshiriki mashindano haya
yaliyodhaminiwa na Oryx, Super Doll, Garda word, Coca Cola, Tanfoam, Hal na
Serengeti ni Lugalo, Dar es Salaam Gymkhana zote za Dar es Salaam, Morogoro
Gymkhana, Arusha Gymkhana, TPC, Moshi na Zanzibar Sea Cliff .
No comments:
Post a Comment