Na Mwandishi Wetu
UTAMU
wa maneno ni kuweza kuyaishi kwa vitendo, ikiwa kinyume huleta dhahama.
Ndivyo imekuwa kwa Simba SC baada ya kupoteza taji la kwanza msimu huu
kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar, katika fainali
ya Kombe la Mapinduzi.
Mchezo
huo ulilindima jana usiku kwenye Uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar,
ambapo Simba ikiwa na mastaa wake tegemeo ilionekana mdebwedo katika
kila idara na Mtibwa Sugar, ambao waliingia fainali baada ya kuichapa
Yanga kwa mikwaju ya penati huku Simba nayo ikiwaondoa mabingwa
watetezi, Azam FC.
Kipigo
hicho kimeacha maumivu na mateso kwa mashabiki wa Simba ambayo
yameongezewa chachandu ya moto na kuchoma zaidi baada ya Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo) kutangaza kuachia
ngazi kutokana na kutoridhishwa na matokeo hayo.
Katika taarifa yake kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mo alisema:
“Baada
ya kulipa mishahara inayofikia Sh4 bilioni kwa mwaka, najiuzulu wadhifa
wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Nitabaki kuwa mwekezaji na
nitazingatia kukuza miundombinu ya soka la vijana.” aliandika Mo.
Mtibwa
ambao walionekana kucheza soka safi na kumiliki mchezo huo, ilipata bao
lake la ushindi dakika ya 38 kupitia kwa Awadh Salum, ambaye alipenya
katikati ya msitu wa walinzi wa Simba.
No comments:
Post a Comment