Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi aonya wananchi wanaojenga mijini bila kufuata utaratibu.
Mhe. Lukuvi
ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Ndachi Kata ya Mnadani jijini Dodoma wakati
akikagua nyumba ambazo zimejengwa bila kufata utaratibu na kukosa vibali vya
ujenzi.
Waziri Lukuvi
alifikia hatua ya kusimamisha ujenzi kwa kuziwekea alama nyumba ambazo ujenzi
wake umekiukwa na kuwaamuru wamiliki kusitisha shughuri zote hadi wafuate
utaratibu.
Hata hivyo Mhe.
Lukuvi amesema Serikali haina mpango wa kubomoa nyumba za wananchi isipokuwa
wananchi wanatakiwa kujenga kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kupata
kibali cha ujenzi.
No comments:
Post a Comment