KIUNGO
mshambuliaji wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, Francis Kahata
amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2019/20, huku Boniface Mkwasa wa Yanga
akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.
Mkwasa
na Kahata walitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzao walioingia nao
fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya
Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Kwa
mwezi huo wa Desemba, Simba ilicheza michezo mitatu, ikishinda yote,
iliifunga Lipuli mabao 4-0, ikaifunga KMC mabao 2-0 na pia ikaifunga
Ndanda mabao 2-0, huku Kahata akiwa sehemu kubwa ya mafanikio ya Simba
kwa mwezi huo na alikuwa katika kiwango bora ikiwa ni pamoja na kufunga
mabao mawili na kutoa pasi za mwisho moja.
Kahata
aliwashinda Hassan Dilunga wa Simba na Bakari Mwamnyeto wa Coastal
Union alioingia nao fainali, ambapo Dilunga naye alikuwa sehemu ya
mafanikio hayo ya Simba akifunga mabao mawili na kutoa pasi ya mwisho
moja, wakati Mwamnyeto alitoa mchango mkubwa kwa Coastal Union
iliyocheza michezo miwili na kushinda yote, ikiifunga Azam FC bao 1-0,
kisha ikaifunga Mbeya City mabao 2-0.
Kwa
upande wa Mkwasa aliwashinda Juma Mgunda wa Coastal na Sven
Vandenbroeck wa Simba, ambapo Mkwasa aliiongoza timu yake katika michezo
minne, akishinda miwili na kutoka sare moja na kupanda kutoka nfasi ya
tisa hadi ya pili katika msimamo. Yanga iliifunga Prisons bao 1-0 na
ikashinda idadi kama hiyo dhidi ya Biashara United na kutoka sare ya bao
1-1 na KMC na ilitoka 0-0 na Mbeya City.
Kwa
upande wa Vandenbroeck aliiongoza Simba kushinda michezo mitatu,
iliifunga Lipuli mabao 4-0, ikaifunga KMC mabao 2-0 na pia ikaifunga
Ndanda mabao 2-0 na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, huku
Mgunda akiiongoza Coastal kushinda michezo miwili, iliifunga Azam FC bao
1-0, kisha ikaifunga Mbeya City mabao 2-0 na kupanda kutoka nafasi ya
sita hadi ya tano.
No comments:
Post a Comment