Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kushoto ) akizungumza na
wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (hawapo pichani) kuhusu kuongeza
ubunifu wa miradi ya kusambaza kugha ya Kiswahili katika mifumo ya Tehama leo jijini Da es Salaam alipotembelea ofisi
hiyo,Kulia ni Katibu Mtendaji BAKITA
Dkt.Selemani Sewangi.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa Dkt.Selemani Sewangi (kulia) akitoa ombi kwa Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kushoto) la
kuomba wizara kuwasaidia fedha za
kununua vifaa vya kufundishia ukalimani alipomtelea
ofisini kwake na kufanya kikao na
wafanyakazi leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kulia) akipokea zawadi ya
Kamusi Kuu ya Kiswahili iliyoandaliwa na
Baraza la Kiswahili la Taifa kutoka kwa Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa Dkt.Selemani Sewangi leo Jijini Dar es Salaam
alipotembela ofisi hiyo kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (kulia) akikagua majengo ya
ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa alipotembelea ofisini hapo leo Jijini Dar
es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu, kushoto ni
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili
la Taifa Dkt.Selemani Sewangi.
Mfasiri Mkuu wa Baraza la
Kiswahili la Taifa Bibi.Vidah Mutasa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyakazi
wenzake kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni
, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi mara
baada ya kumalizika kwa kikao na kiongozi huyo katika ofisi za baraza leo
Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Baraza la Kiswahili la Taifa alipotembelea ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam (watatu
kushoto) ni Katibu Mtendaji Baraza la
Kiswahili la Taifa Dkt.Selemani Sewangi. (Picha na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es
Salaam).
No comments:
Post a Comment