HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 09, 2020

KAIZIREGE, KEMEBOS ZAONGOZA MATOKEO KIDATO CHA NNE

 Wanafunzi katika shule ya Kemebos wakishangili baada ya shule yao kupata kuongoza kitaifa katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne, pili na darasa la nne.


Na Alodia Dominick, Bukoba
 
Kutokana na shule za Kaizirege na Kemebos kuongoza katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne Meneja wa Shule hiyo ametaja mikakati mbalimbali waliyoiweka kama shule ili kupata ushindi.

Meneja wa shule hiyo Eurogius Katiti ametaja mikakati hiyo januari  9 mwaka huu akiwa na mwandishi wa habari alipofika shuleni hapo kujua ni mikakati ipi walijiwekea na ikasababisha wapate ushindi.

 Katiti aliitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na walimu, wanafunzi na viongozi wa shule kuwa timu moja na kumaliza silabasi ndani ya muda pamoja na nidhamu.

Ameongeza kwamba katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu yaliyotangazwa  Januari 9, 2020 shule za Kaizirege na Kemebos imekuwa ya kwanza kitaifa na katika mtihani wa kidato cha pili imekuwa ya pili kitaifa na mtihani wa darasa la nne ya kwanza kitaifa.

"Katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana shule ilikuwa ya tatu kitaifa na leo tumepanda nafasi hivyo tunakibarua cha kuendelea kutetea nafasi hii ili shule yetu iendelee kuongoza kitaifa" Alisema meneja wa shule hiyo Katiti.

Amewaomba walimu, wanafunzi na wazazi kuendeleza ushirikiano ili kuendelea kupata matokeo mazuri shuleni hapo na kuwa wazazi waendelee kuleta watoto wao Kemebos na Kaizirege ili wapate elimu bora.

No comments:

Post a Comment

Pages