HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 06, 2020

MAMA MZAZI WA MWANDISHI ERICK KABENDERA AZIKWA KIJIJINI KWAKE

 Mwili wa Marehemu Verdiana Mujwahuzi ukipelekwa makaburini.
 Jeneza lilokuwa na mwili wa Verdiana Mujwahuzi.
Padre Fortunatus Rutahiwa akiongoza ibada ya mazishi.


Na Lydia Lugakila, Kagera

Safari ya mwisho ya mama wa mwandishi wa habari za kiuchunguzi, Elick Kabendelera anayetuhumiwa na kesi ya uhujumu uchumi yamefanyika leo kwa kuzikwa katika kijiji cha Kashenge katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.

Mwili huo wa mama wa Mwana Habari huyo Erick Kabendera umezikwa katika kijiji cha Kashenge Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera na kusindikizwa na maelfu ya wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

Akiongoza ibada hiyo ya mazishi ya Verdiana Mujwahuzi ambaye ni mzazi wa mwandishi wa habari Erick Kabendera padre Frutunatus Rutahiwa amewaomba watanzania kupendana na kuombeana mema wakati wakiwa hai.

Padre Rutahiwa amesema familia ya marehemu Verdiana Mujwahuzi inapaswa kushikamana na kuishi katika mema katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao kwani ni mipango ya Mungu.

Mazishi hayo yameudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na aliyewahi kuwa mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe, Balozi Khamis Sued Kagasheki huku mbunge wa Kigoma Mjini Mhe, Zitto Kabwe, akitoa salamu za pole katika familia hiyo.

Marehemu Verdiana Mujwahuzi alizaliwa Februari 24 mwaka 1939 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Yeye mbele yetu sisi nyuma yake Mwenyezi Mungu ampumzishe mahala pema peponi Amina.

No comments:

Post a Comment

Pages