Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako pamoja na Mhandisi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)
Rukwa Ding Fubing pamoja na wataalamu wengine wakalipokuwa wakitembelea mradi
wa ujenzi wa chuo hicho mjini Sumbawanga.
Mhandisi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)
Rukwa Ding Fubing pamoja na Mshauri Elekezi wa mradi wa ujenzi wa Chuo hicho Swalehe
Kyabega wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.
Na Mwandishi Wetu, Rukwa
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameagiza kukamatwa kwa
mhandisi wa ujenzi Ding Fubing pamoja na mshauri elekezi wa mradi wa ujenzi wa
Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Rukwa Swalehe Kyabega kutokana na kushindwa kukamilisha
mradi huo kwa wakati huku wakiendelea kusuasua juu ya ukamilifu wa ujenzi huo ambao
ulitakiwa kukamilika 30.12.2019 baada ya kuongezewa siku 100 na hatimae hadi
sasa wamefikia asilimia 52 ya ujenzi.
Prof. Ndalichako
alisema kuwa kimkataba mkandarasi huyo alitakiwa kuthibitisha kwa risiti
matumizi ya shilingi bilioni 1.5 malipo ya awali ya ujenzi kupitia kwa Mshauri
elekezi ambae alishindwa kutoa vielelezo vinavyoonesha utekelezaji wa takwa
hilo la kisheria na kuongeza kuwa mshauri huyo ameshindwa kusimamia matumizi ya
fedha za serikali katika utekelezaji wa mradi huo.
“Mkandarasi aende
akakae ndani mpaka vile vifaa mlivyoruhusu viondoke hapa, mpaka vitakaporudi
ndio muwaachie, kwasababu naona sasa hii inakuwa ni kuchezeana, majibu hamna
kitu ambacho kinachoeleweka, utakwenda kukaa sero hadi utakapotoa maelezo ya
ufasaha juu ya jambo hili, kwasababu huwezi kucheza na serikali namna hii, mara
ya mwisho nilipokuja hapa mlikuwa na vifaa kama vyuma chakavu, mmeleta vifaa halafu mmeviondoa kuvipeleka sehemu nyingine, utakaa ndani hadi vifaa hivyo
vitakaporudi na uwe na watu wa kutosha kufanya kazi, kwasababu tumechoka tunataka
huu ujenzi uishe, wachukue wakae ndani,” Alisisitiza.
Halikadhalika mhandisi
huyo alionekana kuwafanyika kazi wafanyakazi wa mradi huo kwa malipo ambayo
yapo kinyume na mkataba wa serikali huku baadhi ya watendaji wengine wa sekata
ya umeme wakilalamika kufanyishwa kazi bila ya mkataba maalum.
Prof. Ndalichako
aliyasema alipotembelea
ujenzi wa chuo cha ufundi Stadi VETA katika eneo hilo la Kashai lililopo
Manispaa ya Sumbawanga huku akiongozana na watumishi idara ya elimu kutoka
halmashauri mbili za wilaya ya Sumbawanga, Mkuu wa Wilaya hiyo, kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na uongozi wa VETA taifa.
Awali
akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho Mkurugenzi Mkuu wa VETA
nchini Dkt.Pancras Bujuru alisema kuwa mkandarasi huyo tayari amelipwa shilingi 3,507,174,603 ambayo ni sawa na
asilimi 35 ya thamani ya mradi huo na malipo ya mwisho yalikuwa shilingi
330,521,213.79 ambapo alilipwa tarehe 20.12.2019 na kutegemea kuwa baada ya
malipo hayo kasi ya ujenzi ingeongezeka lakini haikuwa kama walivyotaraji.
Mh. Waziri kwa hali hii
mkandarasi amethibitisha uwezo mdogo kutekeleza mradi huu na hatuna imani kama
utatekelezwa kwa wakati kwasababu muda aliopewa na kuongezewa siku 100 vyote
vimekwisha nab ado kazi hazijaweza kuisha kwa muda, kwahiyo tunadhani kwamba
uwezo wake wa kutekeleza mradi hauturidhishi hata sisi, mshauri elekezi
anajukumu la kumsimamia mkandarasi kwa niaba yetu kwasababu tumemuajiri kwa
kazi hiyo, tunajua kwamba amekuwa akitoa maelekezo lakini kumekuwa na udhaifu
wa kuyasimamia kwa kuchukua hatua zinazostahili na kwa muda muafaka naye
tunadhani ana mapungufu,” alisema.
Tarehe
31/8/2019 mkandarasi Tender International alikabidhiwa kiwanja kwaajili ya
kuanza ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika Manispaa ya Sumbawanga pamoja
mshauri Elekezi wa Mradi huo Sky Architect Consultancy Ltd, ambapo mradi huo
ulitegemewa kukamillika mwezi Septemba 2019 huku gharama za mradi huo ikiwa
shilingi 10,700,488,940.05.
No comments:
Post a Comment