Ofisi za Maji Karatu (KARUWASU). |
Na Bryceson Mathias, Karatu
WANANCHI wasio na uwezo wa Halmashauri
ya Wilaya ya Karatu mjini mkoani Arusha, wameilalamikia Serikali kuu wakidai, wamelia
kwa muda mrefu kwamba wanaumizwa na bei kubwa ya Maji ya Shs. 3,000/- kwa ‘Unit’,
hivyo wanaomba iwasaidie.
Wakihojiwa na Mwandishi kwa
Nyakati tofauti Wanyonge hao wamedai, wamechoshwa kununua ‘’Unit’ moja ya Maji
kwa Shs. 3,000/- kwa kuwa bei hivo sasa imekuwa kama msumari wa moto, wakitaka
Serikali ikamilishe Mradi wake wa Arusha Urban Water Supply and Sanitation Authority (AUWSA) ili wafute makovu.
Aidha wamedai, baadhi ya
wananchi waliyopata bahati ya kutumia maji yanayotolewa na Taasisi ya Serikali ya
Karatu Rural Water Supply (KARUWASU) wanafaidi matunda ya Wananchi kwa sababu Unit
Moja yenye Ndoo 50 zenye Lita 20 wananunua Shs. 1,750/-.
Wamelia wakisema, unapokinga
maji yake unapata maji halisi hakuna gesi lakini kwenye maji wanayouziwa Tzs.
3,000/- kwa Unit kwanza unaanza kupa hewa ikifoka halafu baadaye ndiyo unapata
maji jambo ambao linaongeza gharama kwao.
Kutokana na gharama hiyo na
wengine kuambulisha hewa (pesure) kabla ya maji, wameamua kuacha na kulazimika
kununua maji yanyouzwa kwenye kwa Shs. 2,000/- kwa DUMU ambapo wanaona ni nafuu
zaidi.
Kaimu Meneja wa KARUWASU,
Jackson Njau, alipoulizwa wana mpango gani wa kusambaza huduma yao Karatu yote
kama itikio la kusikiliza kilio cha wananchi wanyonge dhidi ya bei kubwa ya
Maji alisema,
“Ninawaomba wananchi wawe
wavumilivu wakati wanakamilisha juhudi za kukamilisha Kufunga Pumpu kwenye
Kisima kilichoko kwenye eneo ulipokuwepo Mti wa wapendao na Ishalah mambo yakienda
sawia huduma yao itakuwa imesambaa Karatu nzima”.alisema Njau aliyekiri gharama
ya bei ya maji wanayoipata wananchi wanaifahamu.
Mmoja wa watendaji wa Maji
Karatu Mjini na Vijijini (KAVIWASU), anayeshughulika na huduma
aliyejitambulisha kwa jina moja la Emma alisema, bei ya Maji yao si Tzs. 3,000/-
kwa Unit pekee! Bali kuna Tzs. 2,000/- kulingana na mahali ambapo maeneo ya
mjini bei ni kubwa kama ilivyotajwa na vijijini ni ndogo.
Aliyekuwa Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, alipowahi kutembelea tanki kubwa la kusambaza maji Karatu ambalo
kwa wakati huo lilikuwa na uwezo wa kusambaza zaidi ya lita 30,000 kwa saa, aliwahi
kutoa uamuzi wilayani humo akisema,
“Ingawa kuna Bodi ya Maji
Karatu Mjini na Vijijini (KAVIWASU), bado kuna haja ya kuundwa chombo kipya
ambacho kinaweza kuunganishwa na KAVIWASU ili kuongeza uwazi”.alisema Pinda
ambapo Serikali ilitangaza mpango wa kuunda Mamlaka ya Maji Karatu ili
kusimamia usambazaji wa huduma hiyo wilayani humo.
Wakati huo huo Januari, 2019 mwaka
jana, Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) aliwahi kumtaka Mkuu wa wilaya ya
Karatu, Theresia Mahongo, kuwatafuta
wataalam wa Serikali, pamoja na wakandarasi waliopata zabuni za kutekeleza
miradi ya maji wilayani humo kufika wilayani bila kukosa ndani ya siku 14.
Wito huo ulikuwa ni kuanzia 28
Januari, 2019 ili kufanyika kikao na wahusika kueleza jinsi walivyosimamia na
kutekeleza miradi ya maji wilayani humo. Aweso alisema hayo katika kikao hicho alichotaka
asitumwe mwakilishi bali wahusika wenyewe.
usudi la Naibu Waziri Aweso ilikuwa kushiriki kikao hicho ili kubaini
changamoto zote za miradi ya maji wilayani Karatu na kutafuta jibu ili maji
safi na salama yawafikie wananchi na wadau wengine kwa wakati kama serikali
ilivyopanga.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya
Karatu, Mahongo, alimwambia Aweso kwamba, miongoni mwa changamoto za miradi ya
maji wilayani hamo ni mapungufu ya kiusanifu. Ambapo alidai hali hiyo ilitokana
na miradi ilipoanza kutekelezwa 2012/2013 haikufanyiwa mapitio ya usanifu upya,
baada ya Mtaalam Mshauri Kampuni ya Tanplanet Njegimi Express kuachishwa kazi
kwa kutokidhi viwango.
No comments:
Post a Comment