MJI
wa Lamadi uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu
unatazamiwa kuwa miongoni mwa miji mikubwa Barani Afrika utakaokuwa
ukiingiza fedha nyingi za kigeni sambamba na kupokea watalii wengi zaidi
kwa mwaka, kutokana na kituo cha michezo cha Maajabu ya Utalii
'Disneyland'.
Hayo
yamesemwa mjini hapana na Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta
ya Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibesse (pichani), wakati
akizungumza na Wajasiriamali katika tukio la kukuza na kuendeleza Utalii
la Lamadi Utalii Festival, kwenye viwanja vya shule ya Itongo, mjini
Lamadi.
Dkt. Kibesse
alisema licha ya kuwa Busega ni Wilaya mpya, wanabahati kupata Mkuu wa
Wilaya mwanamama na mchapa kazi kutokana na kubuni mambo mengi yenye
kuleta tija na fursa za kiuchumi DC Bi. Tan Mwera sambammba na Mkuu wa
Mkoa huo, Anthony Mtaka ambao wamekuwa na mbinu za kuja na fursa zenye
maendeleo.
Amnapo
alieleza kuwa, Lamadi itakuwa ikipokea Watalii wengi na kwa kuwa mwaka
huu mradi huo wa Disneyland unaanza kujengwa, Itakuwa inapokea Watalii
zaidi ya 5,000 kwa mwaka ambapo itakuwa chachu katika kuingiza fedha za
kigeni.
"Tunampongeza
Mkuu wetu wa Mkoa Anthony Mtaka na wasaidizi wake akiwemo DC Tano Mwera
na mwaka huu kituo cha Disneyland kinaanza kujengwa hapo eneo la pori la
akiba la Kijereshi.
Tupopamoja, tutumieni, tuambieni shida zenu tuwafikishie kwa Jemedali Rais, John Pombe Magufuli.
Na
kwa kuwaambia tu, Magufuli anaiependa sana Busega, kwani Mkuu wa
Majeshi anatoka Busega, Gavana anatoka Busega na wapo wengi wanaotoka
Busega mmependelewa kwelikweli, sasa suala sio kupendelewa, tuitumie
hiyo nafasi tujiletee maendeleo na kuliletea Taifa maendeleo kupitia
Busega hii hii ambayo kwa sasa ni mpya lakini itakuwa ni ya kitofauti
hapo baadae." alisema Dkt. Kibesse.
Na
kuongeza kuwa: "Nchi zote za Ulaya, Asia, Afrika na kote, watakuwa
wanakuja Tanzania, lakini watakuwa wanakuja Busega na mtakuwa mnawaona
hapa Lamadi. Nilikuwa huko Marekani Mwezi wa Sita na wa Saba, watalii
karibu 10,000 huwa wanaenda Florida na California kuangalia michezo ya
maajabu ya Disneyland hicho ambacho sasa kinakuja Afrika katika nchi ya
Tanzania, Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Busega" alisema Dkt. Kibesse.
Pia
aliongeza kuwa, Wananchi wa Busega kwa kuwa hawapati fedha za kigeni za
kutosha, wametakiwa kutumia fursa za kuwekeza huduma za Kitalii nyingi
katika mji huo wa Lamadi.
"Tutumieni
fursa za kupata fedha za kigeni 'Dolla', sisi Lamadi hatuzipati sana
Dolla, fursa za mahoteli ni sasa na watakaopata ajira ni wana wa Lamadi,
tunakila sababu ya Busega kujidai". alisema. Dkt. Kibesse.
Akielezea
kwa kina juu ya uchumi wa nchi, matukio kama matamasha na majukwaa ya
kiuchumi katika Utalii, kama ilivyo kwa Lamadi Utalii festival
yanafanyika kwa wakati muafaka kabisa kwa nchi kuhimiza ongezeko la
fedha za kigeni na Utalii ndio bidhaa inayoongoza kuingiza fedha za
kigeni katika nchi hata Wananchi na Rais wanatembea kwa kujidai kwa
sababu nchi ina fedha za kigeni za kutosha.
"Nimetoa mfano kwamba akiba iliyopo sasa hivi hata tukasema watanzania wote tukae hatuzalishi, jambo ambalo haliwezekani.
Hatuzalishi
tumekaa tu tunakula 'bata' tunakunja nne, tunakunywa zetu soda, kajuisi
na kamvinyo kidogo, tunauwezo wa kuimili mikiki yote na uagizaji wa
bidhaa kutoka nje kwa miezi sita.
Ebu
fikiria hiyo hali, kwamba nchi imelala haifanyi chochote, bado inaweza
kuwa 'fanctional' kwa Miezi Sita, sasa hilo sio jambo dogo kwa sababu,
moja nchi haiwezi kulala, inaendelea kila siku. kwa hiyo naomba tutumie
matamatasha haya kuenzi Utalii wa ndani na kuvutia watalii wengi zaidi
na tytaingiza pesa za kigeni." alisema Dkt. Kibesse.
Aidha,
akizungumzia juu ya uwepo wa benki chache kwenye mji huo wa Kiutalii,
alisema kwa muda mrefu Busega ilikuwa na benki moja tu ya Azania, ambayo
ipo katika mji wa Lamadi hivyo amewaomba wadau kuja kuekeza huduma
hizo.
"Busega ni Wilaya mpya. benki nyingi huwa zipo kwenye miji na zikijitanua sana zinaenda kwenye Wilaya.
Busega
imechelewa sana ndio maana nilipoingia kwenye madaraka haya niliyopo
niliizita benki za Kizalendo za CRDB, NMB, POSTA, nikasema haiwezekani
nyinyi benki za kizalendo hampo Busega, wameahidi watakuja, kwani benki
zikiwa nyingi sehemu fulani ndio chocheo la uchumi hivyo nahimiza
mabenki kuja Lamadi ingawa NMB wameanza Nyanshimo.
Lamadi
ndio kila kitu maana nchi jirani wanapita hapa na mzunguko wa
kibiashara hapa ni mkubwa hivyo natumia wasaha huu mabenki yaje
kuwekeza." Alimalizia Dkt. Kibesse.
No comments:
Post a Comment