HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 04, 2020

MASHABIKI YANGA WASHANGILIA SARE DHIDI YA SIMBA

   
Mashabiki wa Yanga.
 Mashabiki wa Simba.
 Golikipa wa Yanga, Faruk Shikhalo, akiruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Januari 4, 2020. (Picha zote na John Dande).
Wachezaji wa timu zote wakiingia uwanjani.
 Chama akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Yanga.
 Deo Kanda akimiliki mpira.
 Hekaheka.


Wachezaji wa Simba wakishangilia.


Na John Marwa 

HATIMAYE shilingi imesimama kwenye Dabi ya Kaliakoo Simba dhidi ya Yanga baada ya mtanange uliowakutanisha leo leo Dimba la Taifa kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL)

Simba walikuwa wa kwanza kuandikisha bao dakika ya 45 lililowekwa kimiani na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penati baada ya kufanyiwa madhambi na Kenvin Yondan. 

Kipindi cha pili dakika ya 47 Deo Kanda aliandikia Simba bao la pili.

 Yanga walirejea mchezo na kusawzisha mabao hayo kupitia kwa Mapinduzi Balama na Mohamed Banka. 

Hadi dakika 90 zinamalizika Simba 2 Yanga 2, kwa matokeo hayo Simba anaendelea kukaa kileleni mwa Ligi huku Yanga wakikwea hadi nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment

Pages