Picha tofauti zikimuonyesha mwanariadha mahiri wa mbio fupi kutoka
Zanzibar, Ally Gulam, akimshukuru Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, baada ya kupewa
fursa ya kusaka kufuzu Olimpiki ambapo atapiga kambi nchini Japan
yatakapofanyika mashindano hayo.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limepanga kumpeleka
kambini mwanariadha, Ally Gulam, nchini Japan hivi karibuni, kwa lengo la
kujiandaa na michuano ya Olimpiki itakayofanyika Julai, mwaka huu.
Michuano ya Olimpiki mwaka huu inatarajia kuanza Julai
24 hadi Agosti 9, itakayo fanyika jijini Tokyo, nchini Japan kwa kushirikisha
michezo mbalimbali kutoka kwa wawakilishi wa mataifa tofauti ikiwemo Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa RT,
Tullo Chambo, alisema wamepanga kuongeza idadi ya wanariadha katika mashindano
hayo mwaka huu kwa mbio ndefu na za
kati.
Hadi sasa wanariadha ambao wanauhakika wa kushiriki
michuano hiyo ya Olimpiki, ni Alphonce Simbu pamoja na Failuna Matanga, ambao
nao wataingia kambini kujiandaa hivi karibuni.
“Mwanariadha mahiri Ally Gulam, tumemuandalia kambi
nchini Japan na hivi karibuni ataelekea huko, lengo ni kuangalia namna gani
Tanzania itavuna idadi kubwa ya medali kulinganisha na miaka iliyopita,”
alisema Chambo.
Alisema joto la mashindano hayo linaendelea kupanda na viongozi
wa RT wanaendelea na mikakati ya kuwaandaa wafukuza upepo wao na kuwaweka kambi
tayari kwa vita hiyo inayosubiriwa kwa hamu.
Chambo, alisema jumla ya wanariadha wawili pekee ndio
wamefuzu kushiriki Olimpiki mwaka huu na waliobaki wanaendelea kusaka muda
utakao wapa tiketi ya kushiriki mashindano hayo.
“Maandalizi yanakwenda vema, kama ambavyo tulisema
awali wale ambao walishafuzu nao ni Simbu (Alphonce), pamoja na Failuna Matanga
wataingia kambini nchini Kenya na ambao bado tunaendelea na mipango mikakati
kujua namna gani watakata tiketi ili wajumuike na wenzao katika maandalizi ya
kwenda kuipepoerusha vema bendera ya Tanzania,” alisems Chambo.
No comments:
Post a Comment