Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akitoka katika nyumba ya Mnufaika wa TASAF Bi. Tatu Salim
wa Kijiji cha Mtipa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida
alipomtembelea kukagua alivyonufaika na mradi wa TASAF. (Picha na Happiness Shayo).
Baadhi ya wanufaika wa
TASAF wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipowatembelea
katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Kijiji cha Mtipa.
Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Bi. Rebeca Mnyawi akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na TASAF wakati wa ziara ya Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika Halmashauri ya Manispaa ya
Singida, Kijiji cha Mtipa .
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Kijiji cha Mtipa .
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na baadhi ya walengwa wa TASAF katika
Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Kijiji cha Mtipa .
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akizungumza na mtoto wa Mnufaika wa TASAF Bi.Tatu Salim
wa Kijiji cha Mtipa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akiwa ameongozana na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Singida kukagua miradi ya TASAF katika Manispaa hiyo, Kijiji cha
Mtipa.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Mnufaika wa TASAF Bw. Issa Ramadhani alipomtembelea nyumbani kwake kukagua namna alivyonufaika na mradi huo.
Na Happiness Shayo, Singida
Serikali imeweka mkakati wa kuboresha huduma zinazotolewa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- ili ziweze kuwanufaisha zaidi Walengwa wa Mpango huo na hatimaye kupunguza umaskini nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika kijiji cha Mtipa,manispaa ya Singida ambako yuko kwa ziara ya kikazi mkoani Singida.
Amesema azma ya serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kuwa wananchi hususani ambao bado wanaishi katika umaskini wa kipato, kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanawekewa mazingira yatakayowawezesha kutumia fursa za Mpango huo kujiletea maendeleo ili hatimaye waweze kuondokana na umaskini.
“Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anayo dhamira ya dhati katika kuboresha maisha ya wananchi, kinachotakiwa kwenu nyie Walengwa wa TASAF ni kumuunga mkono kwa kutumia vizuri fursa zilizoko kwenye Mpango huu ulioanzishwa na Serikali kupitia TASAF” amesisitiza Dkt. Mwanjelwa.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa rai kwa walengwa wa TASAF kuhakikisha kuwa wanatumia ipasavyo huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ikiwamo kuwapeleka shule watoto na kufuatilia mahudhurio yao huku pia akiwataka kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato.
Naibu Waziri huyo wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pia amezungumzia sehemu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambayo inatarajiwa kuanza baada ya kuzinduliwa rasmi na Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli, kuwa mkazo umewekwa katika kuhakikisha kuwa Walengwa wa Mpango wenye uwezo wa kufanyakazi wanatumia nguvu zao katika utekelezaji wa miradi itakayoibuliwa kwenye maeneo yao chini ya utaratibu ujulikanao kama ajira za muda.
“Serikali inasisitiza kila mwananchi mwenye uwezo wa kufanyakazi ni lazima atumia uwezo wake huo katika shughuli za kufanyakazi ili kutoa mchango katika ujenzi wa taifa, hata hivyo wazee na walengwa ambao hawana uwezo wa kufanyakazi kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo maradhi ya muda mrefu serikali kupitia TASAF itaendelea kuwahudumia ” amefafanua Dkt. Mwanjelwa.
Wakitoa ushuhuda wa namna walivyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini baadhi ya Walengwa wameishukuru Serikali ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuwathamini na kuwarejeshea matumaini kupitia Mpango huo unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF. “Tumeweza kuboresha makazi yetu, kumudu huduma kwa watoto wetu katika sekta ya elimu na afya na kuanzisha miradi ya ufugaji wa kuku, mbuzi na ng’ombe baada ya kujumuishwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini” amesema mmoja wa Walengwa Bi. Rebeca Mnyawi mkazi wa eneo la Mtipa nje kidogo ya Manispaa ya Singida. Mhe.Dkt. mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Singida kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF na kukutana na Watumishi wa sekta mbalimbali za umma mkoani humo.
No comments:
Post a Comment