Na Tiganya Vincent
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge imefanikiwa kukusanya kiasi cha
shilingi bilioni 1.835 katika mwaka wa fedha ulimazikia Juni 2019.
Kiasi hicho cha fedha ni sawa na asilimia 87.12 ya lengo la kukusanya
shilingi bilioni 2.106 waliokusudia kukusanya hadi kufikia Juni 2019.
Kauli hiyo
imetolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Martha Luleka wakati
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2018/19.
Alisema
kati ya fedha zilizokusanywa kiasi cha shilingi bilioni 1.354 zilitengwa kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na milioni 480.4 zilipelekwa katika shughuli za miradi
ya maendeleo.
Luleka
alisema kuwa hatua za kinidhamu zilichukuliwa kwa watumishi waliosababisha
kutofika malengo ya kukusanya kwa asilimia 100 ikiwa ni pamoja na kushindwa
kuwasilisha mapato.
Alisema
hatua hizo zilisaidia baadhi ya watumishi kuanza kurejesha fedha za mapato
ambazo walikuwa hawajizipeleka Benki.
Akizungumza
baada ya kupokea taarifa hiyo , Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Peter
Nzalalila aliwataka Madiwani kushirikiana na watumishi katika Kata zao katika
kuhakikisha wanakusanya mapato yote waliyojiwekea kulingana na malengo ya
Halmashauri.
Aidha
aliwataka watumishi waliokabidhiwa jukumu la ukusanyaji mapato ya Halmashauri
ya Sikonge kuhakikisha kila wanapokusanya fedha wanaziwakilisha kwenye akaunti
za Halmashauri zinahusika na mapato.
Alisema
ni marufuku Mtumishi kukaa na fedha kwake pindi anapokuwa ameshakusanya na
kuongeza hatua itawasaidia kuwaondoa katika matatizo ya kupoteza na wakati
mwingine kutumia fedha hizo kinyume cha utaratibu.
No comments:
Post a Comment