HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 01, 2020

WAZEE WA MULEBA WAIPONGEZA CCM

 Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, akizungumza na wazee wa Muleba mkoani Kagera.


Na Lydia Lugakila, Kagera

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, amekutana na kufanya mazungumzo na taasisi ya KWA WAZEE iliyopo Muleba mkoani Kagera.

Katika mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine, taasisi hiyo inayojumuisha wazee 29, 945 kutoka kila kata,  wameipongeza CCM kwa kuanzisha utaratibu wa Mabaraza ya Wazee katika kila ngazi na wao wameahidi kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wazee wote wajiunge kwenye Mabaraza hayo ili changamoto zao zipate urahisi wa kusikilizwa na kutatuliwa kwa pamoja.

Mazungumzo hayo yamefanyika  Januari, mosi  2020 nyumbani kwa Katibu Mkuu Kemondo, Bukoba vijijini.
 

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Bi. Lydia Lugazia akizungumza kwa niaba ya wazee amesema,  "Sisi wazee tuliposikia CCM imeanzisha utaratibu huu wa Mabaraza ya Wazee kwenye kila ngazi, tulifarijika sana kwa kuwa sasa tutapata mahala sahihi zaidi pa kupeleka changamoto zetu kwa pamoja, na kwa kuwa sisi wa Muleba tulisha anza kukaa pamoja chini ya taasisi ya KWA WAZEE, tunaahidi kutoa ushirikiano na kuhamasisha wazee wote tuwe kwenye Mabaraza haya, Ili changamoto zetu zitatuliwe kwa pamoja."

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Bashiru amewahakikishia nia ya dhati ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. John Pombe Magufuli kuunda mabaraza hayo ni kuwa karibu zaidi na wazee na siku zote amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changomoto zenu mbalimbali zikiwemo za Afya zinatatuliwa.

Katibu Mkuu yupo nyumbani kwake Bukoba kwa mapumziko, ambapo anatarajiwa kumaliza mapumziko hayo mapema mwezi Januari, 2020.

No comments:

Post a Comment

Pages