HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 03, 2020

MAMA YAKE ERIC KABENDERA KUZIKWA JUMATATU KATOMA BUKOBA

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, pamoja na waombolezaji wengie wakiaga mwili wa marehemu Verediana Mujwahuzi  ambaye ni mama mzazi wa mwandishi wa habari Eric Kabendera ambaye yupo katika gereza la Segerea akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Shughuli ya kuchimba kabuli ikiendelea huko Katoma mwili wa Verediana Mujwahuzi mama yake na Erick Kabendela utakapohifadhi. (Picha na Alodia Dominick, Bukoba).


  Alodia Dominick, Bukoba
 
Mwili wa marehemu Verediana Mujwahuzi mama yake na Mwandishi wa habari Erick Kabendera utawasili Bukoba Januari 4 kwa ajili ya mazishi.

Mtoto wa marehemu Claudius Kabendera akizungumza  leo na mwandishi wa blog hii amesema kuwa, mwili wa marehemu mama yake utasafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam leo Januari 4 mwaka huu na kuhifadhiwa katika hospital ya Mkoa wa Kagera.

Amesema siku ya Jumapili mwili wa marehemu Verediana utatolewa hospitalini na kupelekwa Rwamishenyi kwenye nyumba yake ambapo alikuwa anaishi wakati wa uhai wake ambapo itafanyika Ibada fupi na mwili huo utalala katika nyumba hiyo hadi siku ya Jumatatu.

Ambapo mwili huo utatolewa na kupelekwa Kashenye kata ya Katoma aneo ambalo ndipo mume wake alikuwa anaishi  na ndipo alizikwa, marehemu Verediana atahifadhiwa katika nyumba yake ya milele siku hiyo ya Jumatatu.

Hata  hivyo maandalizi yanaendelea ambapo wananchi walikuwa wakiendelea kuchimba kaburi huku vifaa mbalimbali kama matofari mchanga maji vikiwa tayari vimewekwa kwa ajili ya ujenzi wa kaburi hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages