HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 17, 2020

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA BALOZI WA UBELGIJI, SWEDEN

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro akisalimiana na Balozi wa Sweeden nchini Anders Sjoberg kabla ya kuanza kwa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, akimfafanulia jambo Balozi wa Ubelgiji nchini, Peter Van Acker, wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. (Na Mpiga Picha Wetu).
 



Na Mwandishi Wetu
 
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker pamoja na Balozi wa Sweeden nchini Anders Sjoberg.

Mazungumzo ya Naibu Waziri, Dk. Ndumbaro pamoja na Balozi wa Ubelgiji yalijikita katika masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji hasa kwenye sekta za Kilimo na Madini.

Balozi wa Ubelgiji, Acker amesema kuwa Ubelgiji itaendelea kuwekeza katika kilimo cha maharage mkoani Kigoma, na kilimo cha Tumbako kinachopatikana katika mikoa ya Tabora, Ruvuma, Katavi na Rukwa.

 " kupitia uwekezaji wa kilimo nchi zetu mbili (Tanzania na Ubelgiji) zimekuwa zikinufaika sawa hivyo ni rai yangu kuona uwekezaji huu unaendelea kutoa fursa za ajira kwa mataifa haya mawaili," Amesema Balozi Acker.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Ubelgiji katika sekta ya Kilimo, Uwekezaji na Biashara.
 
Katika tukio jingine, Naibu Waziri Dk. Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Balozi wa Sweeden nchini Anders Sjoberg, ambapo mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Sweeden nchini Sjoberg amemuahidi Naibu Waziri kuwa Sweeden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa nchi hizi mbili zinapiga hagtua katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Kwa upande wake Naibu Waziri amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendeleza kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano wake na
Sweeden katika Sekta mbalimbali hasa katika wakati huu ambao Tanzania inapiga hatua kuelekea uchumi wa viwanda.

No comments:

Post a Comment

Pages