HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 17, 2020

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA MVOMERO YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA CHUO KIKUU MZUMBE

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwl. Mohammed Utali (kushoto), akiwasili katika viunga vya Chuo kikuu Mzumbe na kupokelewa na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. LughanoKusiluka (kulia).
 Mkuu wa Wilaya, akitoa maelezo kwa msimamizi wa mradi wa ujenzi wa madarasa Injinia Raymond Kweka (alivaa koti refu).
 Mkuu wa Wilaya Mvomero Mwl.Mohammed Utali (katikati) na msafara wake wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Chuo Kikuu Mzumbe baada ya kutembelea na kukagua miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Chuo.
 

Na Mwandishi Wetu
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mvomero ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomer Mwl. Mohammed Utali ameupongeza uongozi wa Chuo kikuu
Mzumbe kwa kuwa na maamuzi yenye tija kwa Chuo na Taifa kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa,, kumbi za mikutano na ofisi za wafanyakazi kwa kutumia mapato yake ya ndani katika ujenzi wa jengo jipya nala kisasa lenye ghorofa nne eneo la Maekani Kampasi
Kuu.

Hayo ameyasema wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi yanayojengwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yakiwa na thamani ya TZS Bil 6.5 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 75. 

Akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalma ya Wilaya ya Mvomero, Utali ameonyesha kutorodhishwa na kaşı ya ujenzi wa mabweni na kulinganisha na Kasi ya ujenzi wa vyumba via madarasa na kumtaka Mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT kuongeza Kasi ya ujenzi kumalizia sehemu ya majengo iliyobaki ili marengo hayo yaweze kutumika Katina mwaka ujao wa masomo kama ilivyokusudiwa.
 
“Nimefururahi sana kuona Chuo Kikuu Mzumbe mnaunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha elimu inaboreshwa kwa kutumia mapato yenu ya ndani kujenga jengo kubwa kama hili. Hii inaonesha Viongozi na watendaji wa Chuo hiki ni watu makini, mnaojali maslahi ya Taifa na Watanzania. Hongera sana Makamu Mkuu wa Chuo na timu yako.” Alisema Mwl.Utali.

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya miradi yote miwili inayoendelea Kampasi Kuu, Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka alisema mradi wa ujenzi wa hosteli umekamilika kwa asilimia 75, na pindi utakapokamilika utatoa fursa ya Malazi kwa wanafunzi 1024 kwa mara moja, huku ujenzi wa vyumba vya. madarasa ukiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1000 kwa mara moja.

Amesema “Chuo kimedhamiria kukamilisha miradi yote mapema iwezekanavyo ili kutoa fursa kwa wadau wengi zaidi kujiunga na Chuo Kikuu Mzumbe, kutimiza ahadi ya Serikali kwa wananchi ya kuongeza fursa za kujiunga na Elimu ya Juu nchini. Alisisitza

Naye Msimamizi wa mradi wa jengo la madarasa wa Kampuni ya SUMA JKT Injinia Raymond Kweka, amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kukamilisha ujenzi huo kwa wakati, kwa kuwa mpaka sasa wapo mbele kulingana na makubaliano ya mkataba na kwamba ujenzi kwa sasa
umefikia asilimia 45 na wana mategemeo ya kukabidhi majengo yote mapema mwezi Julai
2020.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mvomero iko katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya Serikali inayotekelezwa katika Wilaya hiyo, na kuahidi kuendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya miradi hiyo mikubwa kwa kuwa ina maslahi na manufaa makubwa kwa
watanzania na Serikali kwa jumla.

No comments:

Post a Comment

Pages