Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi akitoa
salama za chama katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona.
Baadhi ya wadau wakiwa katika wa kikao cha kupeana mikakati ya kujikinga na corana mkoani Tabora.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Honoratha Rutatinisibwa akitoa ufafanuzi jana
wakati wa kikao cha wadau wa Mkoa huo cha kupeana mikakati ya kujikinga
na corana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri na Kushoto ni
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua jana kikao cha wadau wa Mkoa huo cha kupeana mikakati ya kujikinga na corana.
Na Tiganya Vincent
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewataka wananchi kutopuuza maagizo na
maelekezo ya Rais Dokta John Pombe Magufuli kuhusu kuchukua tahadhari ya
ugonjwa wa homa ya mafua makali unaosababishwa na kirusi kipya aina ya Corona.
Kauli hiyo imetolewa jana na na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwenye
mkutano maalumu wa aliouitisha kujadili mikakati ya kupambana na jinsi ya
kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Aliwataka wananchi wote mkoani humo kuungana pamoja katika utekelezaji
wa mapambano hayo na kuchukua tahadhari ya juu dhidi ya ugonjwa huo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alivitaka vyombo vya habari kutotangaza habari
ambazo hazijathibitishwa kwani kufanya hivyo kutawatia hofu wananchi.
Mwanri alisema kuwa kazi ya vyombo vya habari ni kuchukua taarifa ambazo
zitasaidia kuelimisha umma juu kuchukua tahadhari ili wasiweze
kuambukizwa ama kuambukiza wenzao.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu aliwaasa wananchi
kutekeleza maelekezo ya yote wanayoambiwa na wataalamu wa afya kwani ndiyo moja
ya kinga ya maambukizi ya magonjwa.
Alisema kuwa suala la kinga ni muhimu sana kwani hadi hivi sasa kirusi
kinachoambukiza ugonjwa wa Korona hakijapata tiba.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Honoratha Rutatinisibwa alisema kuwa
wanachi wanapaswa kuzingatia kanuni za afya na usafi kwa kuwa ndio hatua muhimu
ya kujikinga na corana.
Alitoa wito kwa wananchi na taasisi zote zinazotoa huduma za kijamii
kuchukua tahadhari ya kulinda wateja wao ili wasipatwe na maambukizi ya Corona.
Kikao hicho maalumu kimehudhuriwa na Wakuu wa wilaya zote, wananchi,
watendaji, wataalamu wa afya , viongozi mbali mbali wa taasisi za dini na
mashirika.
No comments:
Post a Comment