Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akinawa mikono kabla ya kuingia Kituo cha Afya
Nanyala kilichopo Wilaya ya Mbozi, Kituo hicho kitatumika kutibu wagonjwa Corona
kwa Mkoa wa Songwe endapo watatokea.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela, akizungumza na abiria wa Mabasi katika Kituo cha Mabasi Mlowo kuhusiana na kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela, akizungumza na abiria wa Mabasi katika Kituo cha Mabasi Mlowo kuhusiana na kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameibanisha Kuwa maandalizi ya kukabiliana na
Ugonjwa wa Virusi vya Corona kwa Mkoa wa Songwe yapo vizuri huku akizielekeza Halmashauri
za Wilaya kukamilisha baadhi ya mapungufu yaliyopo.
Brig. Jen. Mwangela
ameyasema hayo jana akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa mara baada ya
kukamilisha ukaguzi wa utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona katika
Halmashauri za Mbozi, Ileje na Halmashauri
ya Mji Tunduma.
Amesema watalaamu wa Afya
ambao watawahudumia wagonjwa wa Corona endapo watatokea Mkoani Songwe tayari
wana mafunzo na Uelewa wa majukumu yao huku Vituo vilivyo teuliwa kwa ajili ya
kuhudumia wagonjwa na washukiwa vimezingatia maelekezo ya Wizara ya Afya.
Brig. Jen. Mwangela
ameongeza kuwa amebaini baadhi ya vituo vya kutolea huduma kwa wagonjwa na
Washukiwa wa Corona vina mapungufu kadhaa ikiwemo uhaba wa maji, umeme na baadhi
ya vifaa tiba na kinga ambapo ameziagiza Halmashauri husika kukamilisha
mahitaji hayo haraka sana.
Wakati huo huo Mkuu wa
Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ametoa elimu ya Kujikinga na
Virusi vya Corona kwa wasafiri, madereva na wafanyakazi wengine wa Mabasi katika
maeneo mbalimbali huku akiwasisitiza kuchukua hatua za tahadhari kwa kunawa
mikono na kuepuka mikusanyiko isiyo ya Lazima.
Naye Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi George Salala amewaagiza
wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha hawajazi abiria kuliko uwezo wa gari
kwakuwa ni kutengeneza mkusanyiko usio wa lazima huku akisema hatua kali zitachukuliwa
kwa watako kaidi.
Kamishna Msaidizi wa
Polisi Salala ametoa angalizo kwa abiria pia kutokubali kupanda mabasi au usafiri
endapo watakuta umejaa kwani mikusanyiko kama hiyo ni mojawapo ya njia ya
kusambaza ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Amesema wamiliki wa mabasi
wanapaswa kuweka maji ya kunawa yenye dawa katika mabasi yao ili kuwakinga
madereva wao na kuwakinga abiria dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona kwakuwa ili
kufanikisha kutosambaa kwa ugonjwa huo inatakiwa jamii yote ishirikiane.
Kwa upande wake Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Hamad Nyembea amesema mpaka sasa maandalizi ya
Utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Corona kwa Mkoa wa Songwe yamefikia asilimia
50 huku mapungufu yaliyobainishwa yatakamilishwa ifikapo mwishoni mwa wiki hii.
Dkt Nyembea ameongeza kuwa
kufuatia agizo la Serikali la kuwaweka karantini siku 14 watu wote walio toka
nchi zenye maambukizi Zaidi ya Virusi vya Corona hadi sasa wamewaweka watu sita
karantini waliotumia mpaka wa Tunduma kutokea nchi ya Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment