NA MWANDISHI WETU
KILA binadamu katika dunia hii ana matatizo yake ya kimaisha, hali ambayo inasababisha kila mmoja kusaka namna ya kufikia malengo kupitia kwa wadau mbalimbali ambao ndio kimbilio la ufanikishwaji huo.
Kwa mazingira ya sasa, wadau wanaweza kutoa msaada kwa jamii
ama mdau mmoja mmoja kwa mujibu wa hitaji la mhusika.
Boniface Mokami (25), mlemavu wa miguu ambaye ni mmoja wa
mfano wa wadau wenye uhitaji wa
kuwezeshwa kwa usafiri aweze kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato
halali katika kujikwamua na umasikini.
Katika mahojiano na Tanzania Daima, Mokami anasema licha ya
kuzaliwa akiwa na hali hiyo a ulemavu, amaanini akisaidiwa kupata usafiri,
ataweza kujishughulisha na kazi mbalimbali za kujitafutia kipato kwa ajili ya
kujikimu.
Mokami anasema, sababu hasa ya kuamua kufikisha ujumbe wake
kwa jamii, ni kupata msaada wa kitendea kazi kimwezeshe kushiriki kazi za
kujipatia kipato cha kuendesha maisha na kuacha kuwa ombaomba.
Hivyo, kilio chake kwa jamii ni kusaidiwa Bajaj
itakayosaidia kufanikisha kipato chake kupitia chombo hicho, kwani ndio
kimbilio lake la kwanza ingawa ana fani nyingine alizozipata katika masomo
yake.
Kwa kuanzia, kuelekea kupatiwa msaada huo wa Bajaj, ameomba
kibali maalum kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ili kufanikisha lengo
lake hilo asiangukie katika kundi la vijana ambao wamekuwa wakishiriki
utapeli.
“Kwa kuwa nahitaji nisaidiwe Bajaj ambayo gharama yake ni
kubwa, nimeanzia kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo ili iwe njia
rahisi ya kufikia malengo ninayo yahitaji,” anasema Mokami na kuongeza:
“Nilijaribu kuomba msaada kwa kuchangisha fedha nyumba kwa
nyumba kwa ajili ya kupata bajaj, nikaona ni bora sualamlangu nilifikishe
serikalini ili niweze kufanikiwa,” anasema.
Mokami anayeishi maeneo ya Changanyikeni, karibu na Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa wazazi wa rafiki yake Noel ambaye ni mlemavu
pia, walifahamiana tangu wakiwa shule wakati huo.
“Ni muda mrefu niko kwa wazazi wa rafiki yangu Noel, kwa
kuwa muda unazidi kwenda naona ni bora nijiongeze kusaka namna ya kujitegemea
na kusaidia wenzangu.
“Kwa haraka, haraka uendeshaji wa Bajaj kibiashara utakuwa
ni msaada mkubwa kwangu,” alisema Mokami na kuongeza
“Fursa ya kuendesha Bajaj ndio kimbilio la haraka ambalo
linaweza kunisaidia katika maisha yangu, hata kutembea kwangu ni kwa shida,
itanisaidia kufanya safari zangu na hapo hapo nitafanikisha kipato change,” anasema
Mokami.
Mokami ambaye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa familia ya
Noel Mokami wa Tarime, mkoani Mara
ambaye hupata shida ya kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutokana
na ulemavu alionao, fani nyingine aliyo nayo ni Graphics Design akiwa na elimu
ya msingi aliyosoma mwaka 2016.
Kabla ya kusomea Graphics, alipata elimu ya sekondari katika
shule ya Moshi Tech kuanzia mwaka 2000, ingawa alishindwa kuendelea na elimu ya
juu baada ya kukosa sifa ya kufika huko.
Baada ya kumaliza Moshi Tech. alirudi nyumbani Tarime, japo
katika miaka minne aliyokuwa masomoni hakuwahi kurejea nyumbani kwa ukosefu wa fedha ambazo zingefanikisha kufika
nyumbani kwao.
Mokami anasema aliishi mkoani Kilimanjaro kwa njia ya kusaidiwa
na wadau kwani wazazi hawakuwa na uwezo kifedha.
Kwa upande wa fani ya Graphics, anasema ameisomea jijini Dar
es Salaam akitokea Changanyike hadi Kimara Temboni alikokuwa akifuata elimu hiyo
ya Graphics akisema moja ya changamoto ni sehemu ya kutekeleza majukumu yake,
inahitajika duka mbalo atauza vifaa vya ofisi na shuleni.
Mokami anasema, hivi sasa wakati akijipanga kwa ajili ya
kusubiri Bajaj hiyo, anajaribu kupita kwa baadhi ya rafiki zake kuomba msaada
huo ili afikie malengo yake.
“Msaada ninaopata kwa sasa kutoka kwa baadhi ya wadau ni
mdogo, hauwezi kufanikisha ununuzi wa Bajaj, nawaomba wadau hapa nchini
wanisaidie ili nifanikishe hatua ninayoifikiria,” anasema Mokami.
Anaweka bayana kwamba alianza darasa la kwanza mwaka
2001-2008, elimu aliyoipata Jeshi la Wokovu Kurasini nafasi aliyoipata kutoka
kwa baba yake mlezi, Francis Machela ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya awali
wilayani Tarime.
Machela ndiye alifanikisha Mokami kujiunga na jeshi la
Wokovu na kupata elimu ambako akiwa shuleni alicheza Mpira wa Meza, mchezo
ambao uko ndani ya damu yake ingawa kwa sasa anafikiria Bajaj kwanza.
Mbali ya ushabiki wake wa mpira wa meza, pia ni shabiki wa
muziki wa miondoko ya RnB na kueleza
kwamba ana mapenzi makubwa na mwanamuziki Young D.
Mokami ni mtoto wa kwanza katika familia yao ya watoto
wanne, wadogo zake wanamtegemea kwa masuala mbalimbali ikiwemo elimu.
Mokami anapatikana kwa namba 0763273650/0652572448
No comments:
Post a Comment