Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi Emelda Salum akizungumza wakati wa semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Arusha ikiwa ni Kampeni ya TCRA , Sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Joshua Mwangasa akitoa mada kuhusiana na makosa ya uhalifu katika mitandao wakati wa semina ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akizungumza wakati akifungua semina ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha ikiwa ni Kampeni ya TCRA Sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka
Baadhi ya Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Arusha wskisoma Mwongozo wa Mtumiaji wa Huduma za Mawasiliano.
Picha ya pamoja kati viongozi wa Dini wa Mkoa wa Arusha na wadau wa Kampeni ya Sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
kuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imechagua kundi sahihi la Viongozi wa Dini kupata elimu ya mawasiliano.
Gambo ameyasema hayo wakati wa semina ya Kamati ya Amani Mkoa Arusha, amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa waumi I juu ya kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.
Amesema watu watumie mawasiliano kwa kuzingatia uzalendo pamoja na kutumia mawasiliano katika kujenga uchumi wa nchi.
"Naamini viongozi wa dini mtafikisha elimu hii kwa ufasaha na kujenga taifa lenye maadili mema katika utumiaji wa mawasiliano"
Amesema Kampeni ya Sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka ni Kampeni ambayo imeanza kwa kundi la Viongozi wa Dini ikiwa ni kundi lenye watu wengi na rahisi kutoa elimu ya kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.
Aidha amesema kuwa katika ukuaji wa sekta ya mawasiliano ni vyema kuwa wabunifu wa kutumia mawasiliano kwa kuhabarishana habari za kujenga maadili.
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Emelda Salum amesema viongozi wa dini kuwa ngazi katika kufikisha elimu kwa haraka kutokana na kuwa na kundi kubwa la waumini wa rika zote.
Mhandisi Salum amesema kuwa semina ya viongozi wa dini italeta mafanikio kwa wananchi kuwa na uelewa namna ya kutumia mawasiliano.
Aidha amesema kuwa Kanda ya Kaskazini itaendelea kutoa Elimu ya Mawasiliano katika Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.
Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania
Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo la kujenga maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali
Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka.
Amesema wakati umefika wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi.
No comments:
Post a Comment