HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 17, 2020

TBA yapongezwa ujenzi wa kiwanda

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa mradi wa nyumba za makazi za Magomeni Kota Benard Mayemba (kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la kiwanda cha kuzalishia matofali ya ujenzi wa mradi huo, jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa mradi wa nyumba za makazi za Magomeni Kota, Benard Mayemba, akieleza hatua iliyo"kiwa ya ujenzi wa nyumba hizo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam. Hadi sasa mradi huo ume"kia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2020. (Na Mpiga Picha Wetu).
Muonekano wa nyumba za makazi ya waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota unaotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambapo ujenzi wake ume"kia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2020.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Dkt. Rashid Chuachua, akikagua mchanga unaotumika kufyatulia matofali katika mradi wa ujenzi wa nyumba za Magomeni Kota, wakati kamati hiyo ilipotembelea hataua zilizo"kiwa za ujenzi wa nyumba hizo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano).
 



Na Suleiman Msuya
 
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa ubunifu ilioufanya wa kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali na kununua mitambo mbalimbali.
Lengo la ujenzi wa kiwanda hicho ni kupunguza gharama za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.
Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso, aliwasisitiza TBA kutumia vizuri sehemu ya eneo lililobaki kwa kujenga majengo na nyumba za biashara ili kuongeza kipato.
Mradi huo ambao ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mwaka 2016 alipowatembelea wakazi  wa Magomeni na kuwaahidi kuwajengea nyumba za kisasa.
“Kama kamati nawapongeza sana kwa kujenga nyumba hizi nzuri kwa wananchi wa kipato cha chini ni imani yangu kuwa kukamilika kwake kutapunguza changamoto ya makazi kwa wakazi waliohamishwa katika eneo hili’
Kakoso alisema TBA inatakiwa irudishe taswira iliyokuwepo kwa washirika wake kwani imefanya vizuri kwa miradi mikubwa inayotekelezwa jijini Dar es Salaam na hivyo kuongeza nguvu kwenye miradi ya mikoa na wilaya zote hapa nchini.
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikw,a alimuahidi Mwenyekiti na Kamati kuwa Serikali itaendelea kuwa karibu na wakala huo ili kuhakikisha unakamilisha miradi kwa viwango na kwa wakati na itaendelea kuijengea uwezo ili iweze kujitegemea.
“Nikuhakikshie Mwenyekiti sisi kama wizara tuko karibu sana na wakala huu na tutahakikisha unaendelea kutekeleza miradi kwa wakati hasa maeneo yanayosuasua’ alisisitiza Kwandikwa.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TBA, Mbunifu Majengo Daud Kondoro, alisema kuwa mradi huo ukikamilika unaweza kuchukua familia zaidi 100 na unatarajia kukamilika mwezi juni, 2020.
Aliongeza mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 70 na kazi zinazoendelea kwa sasa ni kupaka rangi kwenye majengo hayo, kuweka madirisha ya aluminium na kukamilisha ghorofa ya nane ambayo ndio ya mwisho kwa majengo hayo.
Mradi huu wa ujenzi wa nyumba za Magomeni Kota unatekelezwa kwa kutumia fedha za Serikali kwa asilimia mia moja na unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 30.

No comments:

Post a Comment

Pages