Mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite Abdulmusawir Osman, akionesha baadhi ya madini yaliyochongwa tayari kwa matumzi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stanslaus Nyongo (wa kwanza kulia)
akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
waliotembelea Soko la Madini la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu
SOKO la Madini Mkoa wa Dar es Salaam limekusanya Sh. Bilioni 7.616 sawa na asilimia 95.2 ya makadirio ya makusanyo ya Sh. Bilioni nane kwa mwaka wa fedha 2019/2020 unaoishia Juni 30.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Ofisa Madini wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, Ally Maganga alisema makusanyo hayo ni ada ya ukaguzi wa madini, mrabaha, ada ya pango ya leseni na faini.
Alisema pia Tume ya Madini iliyataka masoko ya madini kwa mikoa hiyo, kukusanya Sh. Bilioni 13.157 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na kwamba hadi Februari 2020 masoko hayo yalikusanya Sh. 7,883,886,475.28 sawa na makusanyo ya Sh. 985,485,809.41 kwa mwezi.
"Uwepo wa soko la madini hapa Dar es umeleta mapinduzi makubwa hasa kupunguza kwa kasi vitendo vya utapeli wa madini... tangu kuanzishwa kwa soko hili Julai mwaka 2019 hadi sasa tumefanya biashara kubwa ya madini na kuwasaidia wasafirishaji.
"Kwa kipindi hicho tumepima madini ya vito yenye uzito wa karati 4,887.44 yenye thamani ya Sh. 1,853,514,789.05 na dhahabu kilogramu 46.7 yenye thamani ya Sh. 5,064,825,539.54 wakati Tume ya Madini ilikusanya Sh. 382,620,947.38 ambazo ni mrabaha, tozo za madini na ada ya ukaguzi," alisema Maganga.
Kwa mujibu wa ofisa madini huyo, zipo changamoto za wafanyabiashara katika soko hilo ambazo ni kodi kubwa ya pango ambapo hulipa Sh.24,000 kwa mita moja ya mraba kwenye jengo la Shirika la Nyumba la Taifa.
"Changamoto nyingine ni kukosekana kwa sheria ya kuwalinda masonara na kutokuwepo kwa ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika jengo hilo ili kumpunguzia mzigo mfanyabiashara anayetaka kusafirisha madini.
"Tunataka hapa pawe one stop shop ukiingia na madini unauza unalipa kodi unaendelea na shughuli zako badala ya kuhangaika kuwafuata TRA hii inaleta usumbufu kwa wafanyabiashara wa madini," alisema Maganga.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema Serikali ipo kwenye mchakato wa kutengeneza sera na sheria kwaajili ya masonara hivyo kuwaomba wavumilie kwa muda.
Nyongo alisema suala ka TRA kupata ofisi kwenye jengo hilo lipo mbioni kukamilika huku akisema ni azma ya Serikali kuboresha sekta ya madini na kuimarisha ukusanyaji wa mapato.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Dastan Itandula aliipongeza Serikali kwa kuboresha sheria ya madini na kuanzisha masoko hayo mkombozi kwa mchimbaji wadogo na wakati ambao awali biashara yao ilikuwa ngumu.
"Tumesikia changamoto zenu tutazipeleka bungeni na Serikali itazifanyia kazi kwa haraka kwa kuwa mnafanya mambo mazuri hasa kuondoa utapeli kwenye madini na kukusanya kodi inayotumika kufanya mambo ya maendeleo," alisisitiza Itandula.

No comments:
Post a Comment