Maafisa wa Kiwago Secrurity wakipulizia dawa kwenye maeneo ya hoteli za kitalii
zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni imeendelea kupambana vikali kuthibiti kuenea kwa
virusi vya COVID 19 (Corona) kwa kupuliza dawa katika hotel za kitalii zilizopo
katika Halmashauri hiyo.
Hatua hiyo
ni muendelezo wa mkakati uliowekwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo,
Mkurugenzi Aron Kagurumjuli, Mstahiki Meya Benjamini Sitta, pamoja na Mganga
mkuu Samweli Laizar kwa pamoja, katika kuhakikisha kuwa maambukizi ya
Virus hivyo hayasambai kwa wananchi na hivyo wanaendelea kuwa salama.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo Kaimu Mganga mkuu wa Kinondoni, Dk. Said Hemed amesema
kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama katika kuepukana na
maambukizi ya magonjwa ya mlipuko.
Amefafanua
kuwa mbali na kuthibiti maambukizi ya virusi vya Corona, lakini pia wanachukua
tahadhari ya mlipuko wa homa ya dengu kwakuwa hivi sasa ni kipindi cha mvua.
Ameongeza
kuwa kupuliza dawa katika maeneo hayo ni mahususi kwakuwa wageni wengi hufikia
katika hoteli hizo na kwamba wataendelea kuthibiti kwenye maeneo mbalimbali ili virusi hivyo visienee kwenye makazi ya
wananchi.
“
Tunapopuliza hizi dawa ni kwa malengo mawili, kwanza tunathibiti Corona isisambae
lakini pia tunathibiti homa ya dengue, ukiangalia kipindi hiki ni cha msimu wa
mvua, magonjwa mengi ya mlipuko hutokea , kwa hiyo hii ni njia ya kuwakinga
wananchi wetu wa Kinondoni wasipate maambukizi yoyote” amesema Dokta Hemed.
Aidha
ameongeza kuwa” hotel hizi za kitalii ni maarufu na ndio ambazo zinapokea
wageni wengi, niwasishi sana waendelee kuchukua tahadhari kwakutoa ushirikiano
na Halmashauri yetu ili mlipuko huu usiendelee kwenye maeneo watu.
Awali
Kinondoni ilianza mchakato huo wa kupuliza dawa katika vituo vya daladala,
mwendokasi, na maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo Kanisani na Misikitini
pamoja na maeneo ya wananchi na kwamba bado zoezi hilo linaendelea.
Hadi sasa
zoezi la utoaji elimu kwa wananchi wa Kinondoni linaendelea kwani Kata 20 zilizopo
kwenye Halmashauri zimeshafikiwa sambamba na matangazo ikiwemo kubandika
mabango, kugawa vipeperushi kwa wananchi vyenye ujumbe wa kuelimisha namna ya
kujikinga na virusi vya COVID19 ( Corona).
Imeandaliwa
na Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment