HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 02, 2020

WATUMISHI WASIO KAA KATIKA MAENEO YAO WALIYOPANGIWA MAJUKUMU KAGERA KUKIONA CHA MOTO

Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Projestus Tegamaisho.
 
Na Lydia Lugakila, Kagera

 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Projestus Tegamaisho, amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha anawafuatilia baadhi ya watumishi wanaokwepa majukumu katika halmashauri zao na kukimbilia mijini na kuwafanya wananchi kukosa huduma muhimu kwa wakati.

Hayo yamejiri katika  kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika halmashauri hiyo.

Tegamaisho amesema kuwa wananchi wamekuwa wakikosa huduma muhimu kwa wakati kutokana na baadhi ya watumishi kutopatikana katika maeneo yao walimo pangiwa majukumu yao ya kazi hivyo amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kutowafumbia macho watumishi wa namna hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa baadhi ya watendaji wa halmashauri wamekuwa wakijisahau katika majukumu yao hasa wakikimbilia mijini badala ya kukaa katika maeneo yao kwa ajili ya kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Hata hivyo amesema kuwa hayupo tayari kuona  wananchi wanaangaika katika kukosa huduma muhimu.

No comments:

Post a Comment

Pages