Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamekabidhiwa nyumba tatu na
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zenye thamani ya shilingi milioni 242.
Akikabidhi
nyumba hizo Mkadiriaji Majenzi wa NHC, Anna Bubelwa alisema nyumba hizo
za watumishi wa TFS ni sehemu ya makubaliono ambayo wameingia na wakala
huyo kutatua kero ya makazi.
"Mradi
huu tunaokabidhi leo sisi kama NHC ni kutokana na mkataba tuliosaini
kati yetu na TFS wa kujenga majengo ya watumishi, ofisi za mashamba,
ofisi za TFS wilaya na ifisi za Kanda katika kanda sita zilizopo hapa
nchini," alisema.
Alisema
mradi huu ulianza kutekelezwa Septemba 2019 na umekamilika kwa
asilimia 100 ikiwa ni ujenzi wa nyumba tatu za makazi kwa watumishi
ikiwa moja ni ya Meneja wa Shamba la Miti Rubya yenye vyumba vitatu,
sebule, choo na jiko na nyumba mbili za watumishi wandamizi..
Mhandisi
wa Mradi huo kwa upande wa TFS Kaston Sanga amepongeza serikali kupitia
Wakala wa Huduma za Misitu nchini kwa kutenga fedha kwa ajili ya
Kuboresha nyumba za watumishi katika mashamba ya miti nchini.
"Mradi
huu wa nyumba za watumishi wa Shamba la Miti Rubya ni kati ya majengo
44 yanayotekelezwa na mkandarasi wa NHC ambapo kwa ujumla wake miradi
yote hii imekamilika kwa wasitani wa asilimia 90," alisema Sanga.
Festo
Chaula ni Meneja wa Shamba la Miti Rubya amepongeza juhudi hizi za TFS
za kuboresha makazi kwa watumishi wa wakala wa huduma za misitu.
"Binafsi
ninashukuru sana kukamilika kwa mradi huu maana tumeteseka sana kwa
ukosefu wa nyumba zenye hadhi kukaa watumishi wa Serikali kwani nyumba
tulizokuwa tunaishi hazikuwa na ubora maana zimejegwa mwaka 1982,",
alisema Chaula.
Neema Juma ni Mhasibu wa Shamba la Miti Rubya na moja kati ya watumishi wanaonufaika na mradi huo," alisema.
"Binafsi
ninapongeza TFS kutukumbuka na sisi hatimae leo tumekabidhiwa nyumba
nzuri zenye hadhi ya kuishi watumishi," alisema Neema.
Hata
hivyo TFS wanaendelea na mpango wa kuboresha makazi kwa watumishi
kwenye mashamba ya miti, Ofisi za Kanda, Ofisi za mashamba na Ofisi za
TFS wilaya kote nchini.
No comments:
Post a Comment