HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 26, 2020

Apandishwa kizimbani kwa kudaiwa kusafirisha dawa za kulevya

NA JANETH JOVIN

MKAZI wa Arusha eneo la Wakingori Kisimiri Chini, Kaaneli Akyoo (50) amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.


Akyoo amefikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka yake na upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Mushi.


Ktika hati ya mashtaka imedai kuwa mshtakiwa huyo ametenda kosa hilo Agosti 19, mwaka 2020 huko katika kijiji cha Kisimiri chini wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.


Imedaiwa kuwa siku ya tukio mshtakiwa Akyoo alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilogramu160 huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.


Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande hadi Septemba 7, 2020 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Kwa mujibu wa upande wa Jamuhuri upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika


Juzi Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Arusha walifanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya bangi magunia 116.


Magunia hayo  yalikamatwa mkoani humo katika Oparesheni ya biashara haramu ya bangi iliyofanyika katika Kitongoji cha Karatini Chini Wilayani Arumeru ambapo pia walifanikiwa kimkamta Akyoo  akiwa na gunia tatu na viroba tisa vya bangi vyote vikiwa vimehifadhiwa ndani ya nyumba yake.


Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha mamlaka hiyo, Florence Khambi amesema katika Oparesheni hiyo iliyoongozwa na Kamishna Jenerali James Kaji na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni walifanikiwa pia kukamata viroba tisa vya bangi, gunia moja la mbegu za bangi na misokoto 714 ya bangi.

No comments:

Post a Comment

Pages