Mkuu wa Mkoa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti akikagua timu kabla ya mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya JPM BODA BODA CUP 2020 katika uwanja wa shule ya msingi Kashai Manispaa ya Bukoba.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akionyesha uwezo wake wa kucheza soka kwa kupiga dalizi na danadana kabla ya mtanange kuanza.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akikabidhi jezi kwa moja ya timu kabla ya kuanza mashindano ya JPM BODA BODA CUP 2020.
Na Allawi Kaboyo, Bukoba
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Erisha Gaguti amezindua
mashindano ya mpira wa miguu ambayo yatawashirikisha waendesha pikipiki
maarufu BODA BODA yatakayozijumuisha timu 18 kutoka Halmashauri 6 za
mkoa huo.
Gaguti
ameeleza lengo la mashindano hayo kuwa ni kuwaweka vijana hao pamoja na
kuwapa elimu juu ya ujasiliamali, elimu ya usalama Barabarani pamoja na
elimu ya ulinzi na usalama ili vijana kwa wingi wao waweze kushiriki
katika suala zima la kutunza amani kwani wanakutana na wananchi
mbalimbali wenye taarifa nyingi.
Ameongeza
kuwa vija wa BODA BODA ni muhimu sana kwenye jamii hasa kwenye
usafirishaji lakini pia katika suala zima la kulinda amani maana
hutumika pia baadhi yao kuwasafirisha wahalifu.
"Tumewaka
mashindano haya mahususi kabisa ili kuwafanya vijana kuwa pamoja ili
kuweza kuwajengea uwezo wa ujasiliamali maana kazi hii ya usafirishaji
ina mwisho wake lakini mtu akiwezeshwa katika njia nyingine ataweza pia
kujiendeleza kimaisha na kiuchumi." Ameeleza mkuu wa mkoa Gaguti.
Mashindano
hayo yanazihusisha kata 14 za manispaa ya Bukoba na timu nyingine
kutoka halmashauri ya wilaya Muleba, Karagwe, Missenyi na halmashauri ya
wilaya Bukoba na mchezo wa ufunguzi umezikutanisha timu za Kata ya
Kashai na Bilele.
Aidha
amesema kuwa nje mchezo wa mpira wa miguu yatahusisha mashindano ya
vipaji ya uimbaji kwa wasanii wa mkoa huu ambapo nao pia watapata zawadi
zao.
Mshindi wa kwanza
katika mashindano hayo atapa kitita cha shilingi milioni 3.5, mshindi wa
pili shilingi Milioni 2.5 na mshindi wa tatu shilingi milioni 2.
No comments:
Post a Comment