MWANAFUNZI
wa sekondari Rania Nasser (17)ameandaa maonesho ya picha maarufu kama
–WATU WA TANZANIA yatakayofanyika ukumbi wa Alliance Francie jijini Dar
es Salaam kuanzia Agosti 7 hadi Agosti 12 mwaka huu.
Maonesho
hayo yamedhaminiwa na Ubalozi wa Ufaransa kwa siku tano lengo ikiwa ni
kusaidia kukuza utalii nchini kutokana na picha hizo kubeba maudhui
yanayoonesha shughuli mbalimbali za kiuchumi pamoja na maisha halisi ya
mtanzania yaliyojaa simulizi na historia za Taifa letu
Akizindua
maonesho hayo rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dk.Damas Ndumbaro kwa
niaba ya Serikali ya Tanzania aliahidi kuendelea kuimarisha mahusiano ya
Kidemokrasia na kiuchumi kati yake na Serikali ya Ufaransa ikiwa ni
pamoja na kutumia mahusiano hayo katika kuitangaza Sekta ya utalii
iliyopo nchini ili sekta hiyo iweze kutangazika zaidi katika mataifa
mbalimbali ulimwenguni.
Amesema
“Tanzania na Ufaransa tunamahusiano mazuri kwa muda mrefu hali ambayo
kwa kiasi kikubwa inatunufaisha nchi zote kwenye nyanja mbalimbali hivyo
ni wajibu wetu kama nchi kuyatunza mahusiano haya ili yanendelee
kutunufaisha”.
Baada
ya kuzindua Maonesho hayo Dk.Ndumbaro alipongeza mwanafunzi Rania
Nasser kwa jinsi alivyojitoa muda wake na kupiga picha nzuri
zinazoonesha uhalisia na jinsi watanzania tunavyoishi kwa upendo Amani
na kuamua kuzitoa bure picha zote kwa Bodi ya Utalii Tanzania ili
zitumike kukuza utalii nchni.
“Hongera Rania kwa niaba ya watanzania wote ninakushukuru” amesema Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje,Dk. Damas Ndumbaro.
Kwa
upande wa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier, kwa
nafasi yake pamoja na mambo mengine ameahidi kuendelea kuzitangaza fursa
za utalii zilizopo Tanzania ili sekta hizo ziendeleee kuiamrika na
hatimaye kukuza uchumi wa Taifa.
“Sisi
Ufaransa tutaendelea kushirikiana na Tanzania ili kila ubunifu
unaolenga kuimarisha utalii uweze kuleta maendeleo nchini.” amesema
Balozi wa Ufaransa,Frederic Clavier.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bi Devotha Mdachi akiahidi kuziweka
picha hizo katika vivutio vya utalii nchini na kubanisha kuwa sanaa hii
ya picha ambayo imepewa jina la Watu wa TANZANIA wataiendeleza kwa kuwa
itasaidia mataifa mengi ulimwenguni kufahamu uhalisia wa maisha ya
watanzania vyema na kukuza Utalii.
Naibu Waziri wa Mambo ya nje Dkt Damas Ndumbaro akiwa na Balozi
wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier, pamoja na Mkurugenzi wa
Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bi Devotha Mdachi wakishirikiana na Mwanafunzi wa sekondari umri wa miaka 17 Rania Nasser kukata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua maonesho
ya picha maarufu kama –WATU WA TANZANIA yaliyoandaliwa na mwanafunzi
huyo. Meonesho hayo ya Picha Maarufu kama watu wa Tanzania
yatakayofanyika kwa udhamini wa Ubalozi wa ufaransa katika ukumbi wa
Alliance Francie kwa siku tano mfululizo kuanzi tareh 7 hadi 12.
Mwanafunzi wa sekondari umri wa miaka 17 Rania Nasser akimuonesha baadhi ya picha Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier
Mwanafunzi wa sekondari umri wa miaka 17 Rania Nasser akiongea mbele ya wakati wa kuzindua onesho lake la picha alilolipa jina la –WATU WA TANZANIA linalofanyika katika ukumbi wa Alliance Francie kwa siku tano mfululizo kuanzi tareh 7 hadi 12.
Naibu
Waziri wa Mambo ya nje Dkt Damas Ndumbaro akizungumza kwenye uzinduzi
wa maonesho ya picha yaliyopewa jina la –WATU WA TANZANIA yaliyoandaliwa
na mwanafunzi Rania Nasser yatakayofanyika katika ukumbi wa Alliance
Francie kwa siku tano mfululizo kuanzi tareh 7 hadi 12.
Naibu
Waziri wa Mambo ya nje Dkt Damas Ndumbaro akipokea moja kati ya picha
zilizopo kwenye maonesho ya picha yaliyopewa jina la –WATU WA TANZANIA
yaliyoandaliwa na mwanafunzi Rania Nasser yatakayofanyika kwa udhamini
wa Ubalozi wa ufaransa katika ukumbi wa Alliance Francie kwa siku tano
mfululizo kuanzi tareh 7 hadi 12. Watatu kulia ni Balozi wa Ufaransa
nchini Tanzania Frederic Clavier, na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB Bi Devotha Mdachi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya nje Dkt Damas Ndumbaro akipokea moja kati ya picha
zilizopo kwenye maonesho ya picha yaliyopewa jina la –WATU WA TANZANIA
yaliyoandaliwa na mwanafunzi Rania Nasser.
No comments:
Post a Comment