HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 10, 2020

VIBAKA WAVUNJA NA KUIBA KANISANI

Mchungaji Ernest Majula.

 

 Na Lydia Lugakila, Kagera
 

Vitendo vya kuvunja na kuiba mali za kanisa vimeendelea kushamili katika makanisa mbalimbali mkoani Kagera.
 

Kauli hiyo imetolewa na mchungaji Ernest Majula katika ibada maalum ya harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya jumapili Sunday School na nyumba akina mama BETHANIA iliyofanyika katika mtaa ibosa usharika wa  Burugo dayosisi ya kaskazini Magharibi Mkoani Kagera.

Mchungaji Majula amesema kuwa karibia mwezi mzima makanisa yamevunjwa na kuibiwa yakiwemo ya KKKT, PENTEKOSTE, ROMAN CATHOLIC.

 Matukio hayo yamejiri usiku wa kuamkia jana katika mtaa wa Buzi mkoani Kagera ambapo watu wasiojulikana wamevunja wakachoma sare za Kwaya Kisha kuondoka na vyombo vya Muziki.

Katika hatua nyingine amesema kuwa nako Buyango wamevunja nyumba ya SACCOS na kuondoka na fedha.

Kufuatia hali hiyo mchungaji huyo amewataka wakristo kukemea hali hiyo ikiwemo kutoa taarifa Mara wanapobaini vitendo hivyo.

Hata hivyo mchungaji Majula amewataka wakristo kutokubali kutumika kwa baadhi ya watu wanaoutaka uongozi kwa njia ya Rushwa katika uchaguzi mkuu ujao wa octoba mwaka huu

No comments:

Post a Comment

Pages