HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2020

Romy Jons kuzindua albamu yake Agosti 16

Romy Jons. (Picha na Mpasho News).

 

Na Janeth Jovin


Msanii wa muziki wa Bongo fleva, ambaye pia ni Dj wa Diamond Platnum, anayejulikana kwa jina la Romy Jons amesema kuwa albamu yake mpya ya Changes anayotarajia kuizindua itakuwa ni ya tofauti kwani imeshirikisha wasanii kutoka sehemu mbalimbali Afrika ikiwa Nigeria.

RomyJons anatarajia kuizundua albamu hiyo Agosti 16 mwaka huu ambapo amebainisha kuwa asilimia 80 ya wasanii walioshiriki katika kazi hiyo watakuwepo wakati wa uzinduzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, RomyJons amesema Changes ni albamu yenye lengo la kuwapatia burudani na radha tofauti watanzania na mashabiki wake kwa kuwa imeweza kuwashirikisha wasanii  kutoka Afrika Kusini, Jamaica, Nigeria na hapa nchini.

“Agosti 16, mwaka huu siku ya jumapili, nitaitambulisha albamu yangu katika Hoteli ya Hayatt Regency ambapo asilimia 80 ya wasanii waliopo kwenye albamu watakuwepo hivyo siku hiyo copy na flashi zitapatikana na zitaanza kupatikana rasmi mitaani.

"Hata hivyo baada ya kumaliza uzinduzi nitakwenda katika ukumbi wa Element kukutana na mashabiki zangu ambapo nimekaribisha marafiki zangu tofauti tofauti kutoka nchi tofauti tofauti"amesema RomyJons

Hata hivyo amesema katika albamu hiyo ajapanga kurudisha fedha alizotumia na kuongeza kuwa lengo lake ni kutengeneza kazi nzuri yenye ubunifu na watu waweze kumfahamu.

“Niwaombe radhi mashabiki wangu waliokuwa wakiisubiria Changes ambayo imechelewa kutoka kwa sababu mbalimbali, ila niwashukuru wote waliofanikisha jambo hili, naishukuru WCB ambao wamekuwa wakimsapoti katika kufanikisha jambo langu hili,” amesema

No comments:

Post a Comment

Pages