HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2020

SUA IMEJIANDAA KUFIKISHA MATOKEO YA TAFITI KWA WAKULIMA

Mtaalam wa Maabara ya Udongo katika Idara ya Sayansi za Udongo na Jiolojia, Stevenson Pelegy akitoa elimu ya jinsi ya kupima udongo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dutwa, Mkoani Simiyu walipotembelea banda la SUA.


Prof. Gerald Misinzo akietoa maelekezo kuhusu udhibiti wa panya kwa kutumia mkojo wa panya katika banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wakati wa Maonesho ya Nane Nane, Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
 

Baadhi ya Washiriki kutoka SUA katika Maonesho ya NaneNane Mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao.


Na Mariam Mwayela


Naibu Makamu Mkuu wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Maulid Walad Mwatawala amesema SUA ina Mkakati wa kuhakikisha Matokeo yaTafiti zote zinazofanywa na watafiti zinawafikia kwa wakati.

Akizungumzia kuhusu maelekezo ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Maonesho ya Nane Nane Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Prof. Mwatawala amesema kuwa SUA imeanzasha stashahada mpya ya Tejnolojia na Uzalishaji wa Mbegu (Diploma in Seed Technology and Production) ambayo ni maalumu kwa Maafisa Ugani ili kuwaongezea uwezo katika masuala ya mbegu.


“Stashahada hii itasaidia Maafisa Ugani kusambaza matokeo ya tafiti mbalimbali kwa wakulima ili kuwezakusaidia wakulima hao kulima kilimo chenye tija”, alisema Prof. Mwatawala.


Aidha aliongeza kuwa mbali na kuanzishwa kwa stashahada hiyo inayotarajiwa kuanza mwaka huu pia SUA imekuwa ikifanya mafunzo mbalimbali kuhusu mbegu kwa Maafisa ugani na wakulima kutoka katika Halmashauri naTaasisi mbalimbali nchini.


“Mpaka sasa Halmashauri na Asasi au Taasisi za binafsi zimekuwa zikileta Maafisa Ugani ama wakulima kwa ajili ya mafunzo mbalimbali juu ya ubebeshaji miche ya matunda na jinsi ya kusimamia kitalu cha miche na Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) imekuwa ikiandaa mafunzo mbalimbali kutokana na uhitaji na kwa sasa chuo kiko katika maandalizi ya kuandaa kalenda ya Mafunzo kwa mwaka mzima itakayokuwa inasambazwa kwa wadau mbalimbali ili kuweza kuja na kujifunza.” Alisema Prof.  Mwatawala.


Kuhusu suala la kutumia Kilimo cha kunyunyizia na kuachana na Kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza gharama za kutengeneza Miundombinu Prof. Mwatawala amesema SUA ina Shahada ya Masuala ya usimamiaji wa Rasilimali Maji hivyo kuna haja ya kuangalia ni namna gani watabadilisha ilikuweza kusaidia kutoka katika Kilimo hicho cha umwagiliaji.


Mapema leo Mkoani Simiyu Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaelekeza watafiti wa Sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kuhakikisha wanasambaza matokeo ya tafiti wanazofanya kwa Maafisa Ugani na wadau ili ziweze kuwafikia wakulima.


“Naelekeza watafiti watoe matokeo ya tafiti zao kwa maafisa Ugani ili ziweze kuwafikia wakulima na kunufaika na tafiti hizo,”amesema Mhe. Samia.


Aidha ameiagiza Wizara ya Kilimo kutoa elimu ya utunzaji na uendeshaji endelevu wa miundombinu ya umwagiliaji hususan kujikita katika unyunyizaji na si umwagiliaji ili kupunguza gharama kubwa inayohitajika katika ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kuelekeza kila Mkoa, Wilaya na Halmashauri kutekeleza agizo la kupanda miti na kuhakikisha inamea.


Chuo Kikuu cha Sokoine kinashiriki Maonesho ya NaneNane Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro na Kitaifa Mkoani Simiyu ambapo Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi chagua Viongozi Bora 2020”.

No comments:

Post a Comment

Pages