HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 22, 2020

TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA SASA KUFANYIKA SEPTEMBA 6

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuahirishwa kwa tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania lililokuwa lifanyike Agosti 23, 2020 na kusogezwa mbele hadi Septemba 6. (Picha na John Dande).


 

 DAR ES SALAAM, TANZANIA

 

TAMASHA la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania lililokuwa lifanyika Agosti 23 limesogezwa mbele  hadi Septemba 6 mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 22, 2020 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, amesema kuwa tamasha hilo la kuombea Uchaguzi Mkuu limesogezwa mbele kutokana na shughuli za michezo.

"Tumeandaa Tamasha lenye lengo la kuombea taifa na Uchaguzi Mkuu, tamasha hilo  litafanyika jijini Dar es Salaam, katika uwanja wa Uhuru na hakutakuwa na kiingilio."

"Kuanzia saa tano asubuhi milango itakuwa wazi na saa saba mchana tamasha litaanza rasmi, waimbaji wa nyimbo za Injili, watakao tumbuiza ni pamoja, Bonifasi Mwaitege, Martha Mwaipaja, Rose Muhando, John Lissu na waimbaji wengine wengine zaidi ya 20"alisema Msama

Aidha aliongeza kuwa baada ya kufanyika Dar es Salaam tamasha hilo litafanyika katika mikoa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages