Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa (kushoto), akimuongoza mgeni rasmi Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Mayunga Nkunya, kukagua mabanda ya washiriki wa Maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kabla ya wakati wa kufunga maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Septemba 5, 2020.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH ), Dk. Amos Nungu, akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Mayunga Nkunya, wakati wa kufunga maonesho hayo.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akionesha cheti.
Picha ya kumbukumbu.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya kumbukumbu na kamati ya maandaliazi.
TAASISI za vyuo vikuu nchini zimeaswa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya wamu ya tano za kuongeza fursa za masomo kwa watanzania wengi zaidi bila kuathiri ubora.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Prof. Mayunga Nkunya wakati wa kufunga maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 5.
“Napenda kutoa wito kwa taasisi zote za elimu ya juu nchini kuendelea kuunga mkono juhudi hizi za serikali za kuongeza fursa za masomo kwa watanzania wengi zaidi lakini bila kuathiri ubora.
“Ni wajibu wetu sote kusimamia na kuhakikisha kuwa taasisi zetu zaa elimu ya juu zinakuwa na mifumo imara ya udhibiti ubora inayolenga kuzalisha wataalamu wanaohitajika, ili kufikia adhima hizo vyuo vinahitaji kuwa na viongozi imara, viongozi bora, wenye mtazamo chanya, weledi,wenye maarifa ya kutosha kusimamia sera na miongozo mbalimbali ya elimu ya juu hapa nchini.” Amesema Nkunya na kuongeza kuwa.
“Nimeelezwa na nimeshuhudia leo hii vyuo vingi vimefanya udahili katika maonesho haya jambo ambalo linamuwezesha muombaji kupata urahisi wa kuomba kwa kupewa maelezo yaliyojitosheleza katika chuo husika kwa haraka Zaidi.
“Napenda kutoa wito kwa viongozi wa vyuo vya elimu ya juu kusimamia ukaribu na umakini mchakato mzima wa udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo wa 2020/21, kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima kwa waombaji, wazazi, walezi, wafadhili na wadau wengine wa elimu ya juu.”
Nkunya ameeleza kuwa matarajio yake katika kipindi hiki cha udahili vyuo vitafanya udahili mkubwa ukilinganisha na miaka iliyopia, huku akibainisha kuwa lemgo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa taaasisi za elimu ya juu kubadilishana uzoefu Pamoja na kuonyesha huduma wanazozitoa katika taasisi zao.
“serikali ya awamu ya tano imeendelea kuweka kipaumbele katika kuboresha elimu nchini kwa kupanua fursa kwa watanzania wote katika ngazi zote ikiwemo elimu ya juu.
“Aidha serikali imeendelea kusisitiza vyuo vikuu kutoa elimu bora ili kuzalisha wahitimu wenye uwezo wa kutatua changamoto za jamii, wenye ubunifu na uwezo wa kuhimili ushindani katika soko la ajira kitaifa,kikanda na kimataifa.” Amesema Nkunya.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TCU Charles Kihampa amesema maonesho hayo yamekuwa ya aina yake kutokana na ushindani uliopo katika taasisi za vyuo vikuu nchini jambo ambalo linaongeza hamasa na ubora wa huduma zinazotolewa.
“Natoa wito kwa waombaji wa nafasi za masomo katika taasisi za elimu ya juu kufanya hivyo kwa wakati kabla ya dirisha la usajili halijafungwa septemba 25, hadi sasa ni zaii ya waombaji elfu 30 wamekwisha omba kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.
Nae mwakilishi wa Mawakala wa Vyuo Vikuu nchini Abdul Mollel kutoka Global Link ametoa shukrani kwa serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU kwa kuandaa maonesho bora ambayo yametoa fursa ya kiushindani kwa taasisi shiriki huku akitoa rai maonesho hayo kuendelea kuwepo kwa manufaa makubwa ya elimu ya juu nchini.
No comments:
Post a Comment