HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 28, 2020

KADA CCM AMPONGEZA RAIS MAGUFULI

 


KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya Tanzania Building Works LTD,  Mohamed Noray (kushoto mwenye kofia), akimpongeza Diwani wa Kata ya Manzese jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaama Manumbu Eliam Magafu (kulia aliyesimama) kwa kupata ushindi wa kishindo katika hafla fupi ya diwani huyo kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumuamini kumpigia kura kwa wingi. (Na Mpiga Picha Wetu).

 

NA MWANDISHI WETU


Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Building Works LTD Mohamed Noray amesema serikali ya awamu tano chini ya Uongozi wa Rais John Magufuli imefanya kazi kubwa katika sekta ya ujenzi hasa miundombinu ya barabara.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kuhudhuria sherehe zilizoandaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Manzese kutokana na ushindi wa kishindo walioupata katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Amesema yeye aligombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Ilala lakini hakufaniliwa kushinda lakini ameendelea kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa chama hasa kutokana na kazi kubwa anayoifanya Rais Magufuli ikiwemo sekta ya ujenzi.

Amesema ni lazima wanaccm waendelee kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa chama ili kumsaidia Mwenyekiti wao ambaye ni Rais John Magufuli

Amesema yeye akiwa kama Mkurugenzi  wa Kampuni inayo jishugjulisha na masuala ya ujenzi  katika.maeneo mbalimbali nchini ameona jinsi kazi kubwa ya ujenzi ilivyofanyika yakiwemo madaraja na barabara.

Amesema ni lazima wanaccm kujivunia uongozi wao kutokana na mazito wanayoyaona ili kusaidia kueneza mambo mengi mazuri kutokana na umuhimu wake kwa nchi 

Baadhi ya viongozi wa CCM walisema chama chao kitaendelea kupata ushindi wa kishindo katika chaguzi zote zijazo kutoka na kazi nzuri ya serikali ya awamu ya tano


No comments:

Post a Comment

Pages