HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 28, 2020

Naibu Waziri wa Maji azipongeza RUWASA na AUWASA


Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akimtua mama ndoo ya maji mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa King’ori wilayani Arumeru.

 

Na Eavristy Masuha

 

Naibu waziri wa maji,mhahindisi Maryprisca Mahundi amepongeza juhudi zinazofanywa na Wakala wa Usmbazaji Maji Vijijini (RUWASA) mkoani Arusha na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Arusha( AUWASA) kwa jitihada kubwa ya kutoa huduma kwa wananchi.

Naibu Waziri  ametoa pongezi hizo katika kijiji cha King'ori, wilaya ya Arumeru wakati wa uzinduzi wa mradi wa Maji wa King'ori unaotekelezwa na kusimamiwa na RUWASA. Mradi ambao utekelezaji wake umegharimu shilingi bilioni 1.5, ambao tayari umekamilika.

Amesema RUWASA na AUWASA imekuwa ikijituma kutekeleza miradi na kutoa huduma kwa wananchi. Ikiwamo mradi huo wa King'ori ambao utawanufaisha wananchi takribani 3,410 waliopo katika vijiji vya King'ori na Muungano, huku akiweka wazi kwamba huo ni wajibu  ambao kila kiongozi na mtumishi wa umma anatakiwa kutekeleza.

" Nikuhakikishie Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya(Mheshimiwa Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru), hoja yako ni ya msingi kabisa, kwasababu hata Mimi nimejionea kwamba chanzo cha Maji kinatosheleza. Nitahakikisha fedha zinapatikana mapema ili huduma hiyo ya maji ifikishwe kwa wananchi," Amesema Naibu Waziri.

Awali Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Jerry Muro katika taarifa yake kwa Naibu Waziri aliomba Serikali ione umuhimu wa kupanua mradi huo ili huduma iweze kufika katika vijiji jirani na mradi huo vikiwemo vijiji vya Mareu na Oldonyong'iro ambavyo navyo vina changamoto ya uhaba wa Maji safi na salama.

Miradi mingine iliyotembelewa na Naibu Waziri katika ziara yake ya mkoani Arusha ni Imbaseni na mradi unajulikana kama Mradi wa Vijiji vitano ambao unafadhiliwa na DFID na kusimamia na kampuni ya water AID ukilenga kutoa huduma ya maji na kupunguza madini ya Fluoride kwenye maji.

No comments:

Post a Comment

Pages