Meneja Mwandamizi Idara ya biashara za Kadi wa Benki ya NMB - Manfred
Kayala (katikati) akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya pili ya
Promosheni ya Mastabata IsiyoKikawaida iliyochezeshwa jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Meneja
wa Kitengo cha uzalishaji Kadi wa Benki ya NMB -Sophia Mwamwitu na
kulia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha - Rasuli Masudi.
Kampeni hii ya miezi mitatu ilizinduliwa Novemba 24 mwaka huu, ambako
zawadi mbalimbali zinatolewa zikiwamo za pesa , simu janja ‘smartphone’,
jokofu, runinga pamoja na safari ya kwenda kupumzika Zanzibar,
Serengeti na Ngorongoro.
Droo ya pili ya kampeni, imefanyika Makao Makuu ya NMB, jijini Dar es
Salaam, chini ya usimamizi wa Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania (GBT), Rasuli Masudi, aliyewahakishia washiriki na washindi
mchakato unaozingatia sheria zote kuwapata.
Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara
za Kadi wa NMB, Manfredy Kayala, alisema katika kipindi chote cha
kampeni hiyo, watakabidhi zawadi kwa jumla ya washindi 40
watakaojishindia fedha taslimu 100,000 kila wiki.
Pia, alifafanua kuwa NMB MastaBata itawazawadia washindi 15 simu janja
aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye thamani ya Sh. 2,480,000 kila
mwezi, pamoja na zawadi kuu itakayotolewa katika fainali ya kuhitimisha
kampeni hiyo.
"Zawadi kubwa kwenye kampeni hii ni ile ya washindi 15 pamoja na wenza
wao kushinda safari ya utalii wa ndani iliyolipiwa kila kitu na NMB,
ambapo mshindi na mwenza wake watapata nafasi ya kutembelea Zanzibar,
Serengeti na Ngorongoro.
"Aidha, washindi wa fainali watawapa ruksa ya kuchagua utalii wa ndani
au kuchukua zawadi mbadala kama runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu,
Jokofu la Milango Miwili, Kompyuta Mpakato, Simu Janja (Samsung A70),
Water Dispenser na Microwave," alisema Kayala
Kwa upande wake, Masudi kutoka GBT, aliwatoa shaka wateja wa NMB
wanaoshiriki kampeni ya NMB Mastabata Siyo akisema mchakato wa kutafuta
na kutangaza washindi, unafanyika kisheria chini ya bodi hiyo na kwamba
hakuna ubabaishaji katika hilo.
Aliwataka wateja wa NMB waendelee kufanya manunuzi kutumia kadi za NMB
Mastercard, Mastercard QR, pamoja na POS ili kushiriki kinyang'anyiro
hicho mara nyingi wawezavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi za
wiki, mwezi na hata 'grand finale' Februari
2021.
No comments:
Post a Comment