Chama cha ACT Wazalendo kimepongeza hatua ya utiaji saini Mkataba wa Maelewano baina ya Oman na Serikali ya Umoja wa Kitaifa SUK juu ya ujenzi wa Bandari Jumuishi huko Mangapwani, Kaskazini mwa Zanzibar.
Katibu
wa Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano Kwa Umma wa Chama Cha ACT
Wazalendo, Ndugu Salim Bimani amesema."Hii ni hatua kubwa na muhimu kwa
ajili ya uchumi na ukuaji wa Zanzibar inayoongozwa na Rais Dk Hussein
Mwinyi".
Utiaji saini wa
makubaliano hayo yaliyofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi Bwana, Amour Hamil Bakari na kwa upande kwa
upande wa Oman alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji cha
Oman Sheikh Mohammed Al-Tooqi ambaye aliongoza ujumbe kutoka Mamlaka
hiyo ya Oman.
Chini ya makubaliano hayo Oman imeweka nia kujenga
bandari kadhaa kama vile ya mizigo na makontena, Petroli na gesi, Uvuvi
na pia kuwepo chelezo kwa ajili ya matengenezo ya meli za ndani na nje
katika ukanda huu.
Pia
kuweko eneo la viwanda, eneo la biashara na makaazi ya kisasa, imeelezwa
na Rais Mwinyi amesema huu ni mwanzo mzuri kwa Zanzibar " Lengo letu ni
kuleta mabadiliko makubwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu na fursa na
faida kwa watu wote."
Chama
cha ACT Wazalendo kinawataka wananchi wote wasimame na Serikali ya
Umoja wa Kitaifa kwa umoja wao iki kuitia hima na shime katika kuijenga
Zanzibar yetu "Kila tukishikamana ndio tutaipa nguvu Serikali ya Umoja
wa Kitaifa kufanya kazi na nchi mbali mbali na makampuni mbali.
Tunaamini mazingira mazuri zaidi yatandikwa kushawishi wawekezaji
zaidi," alisema Bimani
Pia
Bimani aliishukuru Serikali na watu wa Oman kudhihirisha uhusiano na
udugu wa kweli kwa Zanzibar kwa kuweka nia ya mradi huo utakaotoa ajira
kwa maelfu.
Itakumbukwa Oman imefanya miradi kadhaa
kikiwemo kilichokuwa Chuo cha Afya cha Mbweni na sasa ni sehemu ya Chuo
Kikuu cha Zanzibar SUZA na pia Oman inasimamia ujenzi na uhifadhi wa
Jengo la Beit Al Ajaib ambalo sehemu yake kubwa iliporomoka Disemba 25,
2020.
No comments:
Post a Comment