Meneja kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Sophia
Mwamwitwa akizungumza kwenye droo ya MastaBata leo katika ofisi za Benki
ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi
ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na
kulia ni Afisa Huduma kwa Wateja, Yvette Nkhoma. Hii ni droo ya wiki ya
sita hadi sasa tumepata washindi 200 waliojishindia shilingi 100,000/-
kila mmoja.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Yvette
Nkhoma (kulia) akibofya kitufe kumpigia simu mmoja wa washindi wa droo
ya Mastabata si Kikawaida, alioibuka mshindi katika droo ya wiki ya sita
iliyoendeshwa leo. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na katikati ni Meneja kitengo cha Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa.
Afisa Huduma kwa Wateja wa
Benki ya NMB, Yvette Nkhoma (kulia) akizungumza na mmoja wa washindi wa
droo ya Mastabata si Kikawaida, alioibuka mshindi katika droo ya wiki
ya sita iliyoendeshwa leo. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania, Pendo Mfuru akisimamia droo hiyo na katikati ni Meneja kitengo cha Biashara ya KadiBenki ya NMB, Sophia Mwamwitwa.
DROO
ya sita ya Kampeni ya NMB MastaBATA, inayoendeshwa na Benki ya NMB,
imefanyika jijini Dar es Salaam, ambako washindi 40 wamepatikana na
kufanya idadi yao tangu kuanza kwake Novemba 2020, kufikia 240.
NMB
MastaBATA, ni Kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa Novemba 24, 2020
na itadumu hadi Februari mwaka huu, ambako zawadi mbalimbali zinatolewa
zikiwamo pesa, simu janja, jokofu, runinga na safari ya kwenda kupumzika
Zanzibar, Serengeti na Ngorongoro.
Droo
hiyo imesimamiwa na Pendo Albert, kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania (GBT), ambako washindi wamejinyakulia Sh. 100,000 kila mmoja,
kigezo cha ushiriki kikiwa ni matumizi ya Kadi za NMB Mastercard na
Masterpass QR.
Akizungumza
kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, Meneja wa Idara ya Kadi ya NMB,
Sophia Mwamwitwa, alisema jumla ya washindi 200 walishapatikana katika
droo tano za kila wiki, na kwamba kampeni nzima inalenga kuzawadia
washindi 400.
Aliongeza
kuwa, ukiondoa droo za kila wiki, pia NMB MastaBATA imewazawadia jumla
ya washindi 12 kati ya washindi 15 wa droo za kila mwezi ambao wao
wamekuwa wakijishindia simu janja aina ya Samsung Galaxy Note20, yenye
thamani ya Shilingi Mil. 2.4
"Wito
wetu kwa wateja wa NMB wenye kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR,
kufanya manunuzi na malipo mbalimbali ili kujiwekea nafasi ya kushinda
droo zijazo za kila wiki, kila mwezi na ile zawadi kuu ya Grand Finale,"
alisema Mwamwitwa.
Aidha,
zawadi kuu ya Grand Finale ambayo ni utalii Zanzibar, Ngorongoro ama
Serengeti, inawapa washindi uhuru wa kuchagua zawadi mbadala kama
runinga iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, Jokofu, Laptop, Simu (Samsung
A70), Water Dispenser na Microwave.
Kwa
upande wake, Pendo, Ofisa wa GBT, aliwataka wateja wa NMB kuendelea
kutumia kadi zao ili kujishindia zawadi zinazotolewa na NMB MastaBATA,
na kwamba mchakato wa kuwapata washindi unafanyika kwa kufuata sheria na
taratibu.
No comments:
Post a Comment